MWALIKO WA WADAU KUTOA MAONI MBELE YA KAMATI YA BUNGE YA KATIBA SHERIA NA UTAWALA BORA KUHUSU MUSWADA WA SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA YA NCHI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MWALIKO WA WADAU KUTOA MAONI MBELE YA KAMATI YA BUNGE YA KATIBA SHERIA NA UTAWALA BORA KUHUSU MUSWADA WA SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA YA NCHI

(THE CONSTITUTIONAL REVIEW BILL, 2011)
Kwa mujibu wa Kanuni ya 114(9) ya kanuni za kudumu za Bunge, kamati ya Bunge ya Katiba, sheria na Utawala Bora inawaalika wananchi na wadau wote kushiriki katika mkutano wa kupokea maoni kuhusu Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya katiba ili kupata maoni na ushauri wao kwa ajili ya kuboresha Muswada huo.

Mikutano ya kupokea maoni hayo itafanyika tarehe 7, 8 na ikibidi tarehe 9 April, 2011 Mjini Dar es salaam na Dodoma kama jedwali hapa chini linavyoonyesha:

S/N                 SIKU                            MKOA                      UKUMBI                   MUDA
               7 – 8/April/2011                 Dar es salaam               Karimjee           Saa 3 Asubuhi
               7 – 8/April/2011                    Dodoma                      Msekwa

Kwa taarifa hii, wananchi wote kwa ujumla wanaalikwa kushiriki kwenye mikutano hii kwa ajili ya kutoa maoni yao kama inavyoonekana katika jedwali hapo juu.

Imetolewa na:

Ofisi ya Bunge
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa
Dar es Salaam
5 Aprili 2011

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages