Askari wakimdhibiti mmoja wa waandamanaji katika tukio hilo leo asubuhi mjini Morogoro.
NA DUNSTANN SHEKIDELE, MOROGORO
JESHI la polisi mkoani hapa, leo asubuhi limetembeza kichapo kikali kwa madenti wa shule za msingi na sekondari pamoja na madereva na makondakta wa daladala huku chanzo cha vurugu hizo kikielezwa kuwa ni mgomo wa madereva daladala wakipinga ushuru mkubwa wanaotozwa na halmashauri ya manispaa ya Morogoro.
Mgomo huo ulisababisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kukosa usafiri wa kuelekea mashuleni hivyo kwa pamoja wanafunzi hao waliamua kuandamana kupeleka malalamiko yao kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Luteni Kanali Mstaafu, Issa Machibya.
Hata hivyo wakati madenti hao wakiwa katika maandamano, walikutana na gari la polisi lililowataka watawanyike mara moja lakini baadhi yao walionekana kukaidi amri hiyo ndipo jeshi hilo lilipoamua kuwatawanya kwa nguvu.
Kufuatia hali hiyo baadhi ya madenti waliamua kupambana na polisi kwa kuwatupia mawe huku madenti wengine wakiziba barabara kwa kutumia mataili ya magari, jambo ambalo lilionekana kuwapandisha hasira vijana hao wa IGP Mwema.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)