MFUMO MPYA WA MIKOPO KWA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU KUANZA KUTUMIKA LEO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MFUMO MPYA WA MIKOPO KWA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU KUANZA KUTUMIKA LEO

Mwanaidi Abbas
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), imezindua rasmi mfumo mpya wa uombaji wa mikopo kupitia njia ya mtandao, inayoanza kutumika rasmi leo.

Akizungumza na waandishi wahabari jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Bodi hiyo, George Nyatega, alisema utaratibu huo mpya, utaanza kutumika kwa wanafunzi wa mwaka wa masomo 2011 /2012.

Alisema hatua hiyo itarahisisha kazi kwa bodi na kuzuia tatizo la kupotea kwa fomu za waombaji kama ilivyokuwa huko nyuma wakati waombaji, walipokuwa wakituma fomu zao kwa njia ya posta.

"Utaratibu huu utapunguza kazi na gharamza za waombaji hususan waliko mikoani, ambao wamekuwa wakitumia muda mwingi kufika hapa," alisema Mkurugenzi huyo.

Alisema hatua ya bodi kufikia uamuzi wa kutumia njia hiyo, imesukumwa na ongezeko la waombani na maendeleo katika teknolojia ya mawasiliano.

Nyatega alisema hatua hiyo itaboresha utendaji na kuongeza ufanisi katika utoaji wa mikopo kwa wanafunzi.Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Profesa Anselm Lwoga, alisema kkuanzishwa kwa mtandao huo kutawafanya wanafunzi,kutopanga tena foleni katika bodi ya mikopo, wakisubiri fomu kama ilivyokuwa awali.

Alisema tayari bodi imeshasambaza vipeperushi katika ila ofisi za wilaya ili kuwawezesha waombaji, kujua namna ya kutumia mtandao huo.
CHANZO: MWANANCHI

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages