KIBAKA AOKOLEWA NA ASKARI WA ULINZI MIKONONI MWA RAIA WENYE HASIRA KALI MARA BAADA YA KUPORA SIMU - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

KIBAKA AOKOLEWA NA ASKARI WA ULINZI MIKONONI MWA RAIA WENYE HASIRA KALI MARA BAADA YA KUPORA SIMU

Askari wa Ulinzi wa Kituo cha Mafuta cha Big Bon Kariakoo, wakimuweka chini ya ulinzi kijana ambaye hakuweza kufahamika jina lake, aliyekamatwa baada ya kumchomolea simu ya mkononi, mwanamama aliyekuwa katika harakati za kugombea usafiri katika Kituo cha Msimbaji Dar es Salaam leo mchana. Wananchi wenye hasira kali walimuadhibu kijana huyo kwa kumpiga na mawe, virungu na kusababisha kutokwa na damu mdomoni. Hapa ni raia wakitoa kipigo cha mbwa mwizi kwa kijana huyo, nyuma yake ni mwanamama ambaye kwa kweli sikuweza kujua alichokuwa akikifanya nyuma ya kijana huyu, sijuli alikuwa akimsachi ama vipi. 
Habari/Picha Na Mdau Dar.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages