IMANI ZA KISHIRIKINA MJI KASORO BAHARI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

IMANI ZA KISHIRIKINA MJI KASORO BAHARI



Paka mwenye ungo na nguo nyeusi amekufa papo hapo baada ya kinachosemwa  kudondoka kutoka kwenye paa ya nyumba ya mkazi wa mtaa wa Mwembeni kata ya Chamwino,manispaa ya Morogoro Amina Ally (55)  tukio  lilohusishwa na imani za kishirikina.

Akizungumzia  tukio hilo Mganga wa tiba za asili kutoka mkoa wa Tabora, Mfaume Ally alisema Tukio hilo limetokea machi 30 mwaka huu majira ya saa 10 afajili katika Manispaa ya Morogoro.

Mfaume alisema paka mwenye ungo na nguo nyeusi alidondoka katika nyumba ya mteja wake na kufa papo hapo baada ya jaribio la kudhuru kwa njia za giza kushindikana kutokana na nyumba hiyo kuwa na kinga madhubutu.

Alisema kuwa paka huyo licha ya kuwa na ungo na nguo nyeusi  (kaniki) ambayo alifungwa tumboni pia alikuwa na vitu vingine vikiwemo salafu za senti tano na senti 10 fedha ya zamani za Tanzania zilizochomekwa kwenye ungo huo  pamoja na chupa nyekundu ikiwa imefungwa katika ukingo wa ungo.(Picha:Mdau  wa Morogoro)kupitia Kwa Mjengwa

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages