Na Wilbert Molandi
MIGOGORO inayoendelea kuitafuna timu ya Yanga, imeelezwa kuwa sababu kubwa ya kuchelewa kukamilika kwa mipango ya kutua nchini kwa klabu za Livepool na Tottenham Hotspurs za England.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Africa Aid inayofanya mpango wa kuzileta klabu hizo nchini, Davies Mosha amesema migogoro inayoendelea ndani ya timu hiyo yenye maskani yake makutano ya mitaa ya Jangwani na Twiga imesababisha ashindwe kuelekeza nguvu zake katika kusimama ujio wa timu hizo.
“Najua wapenzi wa soka wana kiu ya kuziona Liverpool na Spurs, naomba niwatoe hofu kwa kuwaambia klabu hizo lazima zitue nchini kwa ajili ya kutoa burudani.
“Mchakato wa kuleta klabu hizo umesimama kwa muda kutokana na migogoro ya Yanga, lakini mara baada ya kumalizika nitakamalisha baadhi ya mambo kwa ajili ya kukamilisha ujio wao,” alisema Mosha.
“Kuna mgogoro unaoendelea kati yangu na baadhi ya viongozi wa Yanga ambao siwezi kuuzungumzia katika kipindi hiki,” alisema Mosha ambaye amedai kuwa mpango wake ni kuzileta klabu kubwa za soka duniani kila mwaka.
Tayari Mosha kupitia kampuni yake ameanza mazungumzo na timu hizo za England lakini Championi limegundua ni kwa msaada wa Shirika la Misaada ya Watoto la Umoja wa Mataifa (Unicef).

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)