WATU wengi hufikiri kwamba albino ni binadamu tu. Hii si kweli. Kiumbe chochote kuwa albino ni kukosa rangi ya asili inayotakiwa kuwa juu ya ngozi. Hii ni pamoja na wanyama, mimea na viumbe vingine hai.
Kukosekana kwa rangi hiyo ya asili hufanya kiumbe husika kuwa na rangi nyeupe ambayo haifunikwi na kitu chochote. Hali hiyo hukifanya kiumbe husika kuwa katika hatari ya kukumbwa na madhara mbalimbali, yakiwemo magonjwa, hususan kwa binadamu na wanyama.
Pichani ni chatu albino, akiwa hana rangi ya asili. Kwa kawaida huwa na rangi ya kijani. Hivyo, wenye kufikiri kwamba albino ni binadamu tu, wafahamu tangu sasa kwamba hali hiyo huvikumba viumbe vingine vyovyote hai.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)