MSIBA CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM) NA ISHOZI GERA BUKOBA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

MSIBA CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM) NA ISHOZI GERA BUKOBA

   LJ B  LOG inapenda kutoa pole kwa Wanafunzi Wote Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) familia,ndugu, jamaa na marafiki wote Juu Ya Msiba Wa Ndugu,dada,Mwanafunzi mwenzetu Eva Katabalo Ambaye amepoteza maisha jana Majira ya saa nne asubuhi Mara baada ya Kuanguka Ghafla wakati  akielekea Bafuni.
      Eva Katabalo alikua Ni Mwanafunzi wa Mwaka Wa Tatu Katika Chuo Kikuu Cha Dodoma kutoka Kitivo Cha Sayansi Ya Jamii na Sanaa ya Lugha.
      Mpango Wa Mazishi Unaendelea Na muda si mrefu mwili wa marehemu utawasili chuoni hapa katika ukumbi wa Chimwaga kwa ajili ya wanafunzi na wafanyakazi kuuaga.Shughuli ya kuaga mwili wa marehemu utafanyika katika ukumbi wa chimwaga uliopo chuoni hapa huku ikianza na misa ya kumsalia marehemu na baadae kushafilishwa kuelekea kwao Gera Ishozi Bukoba Kwaajili Ya Mazishi.
       Tunapenda Kutoa Pole Kwa familia yake ambayo kwa sasa ipo katika kipindi hiki kigumu kwa kuondokewa na Ndugu yao Mpendwa.Tunamuomba Mwenyezi Mungu Awalinde Ndugu, jamaa, marafiki wa marehemu katika kipindi hiki kigumu na kuwapa subira.
        LJ BLOG inapenda kutoa pole kwa wanafunzi wote wa Chuo Kikuu Cha Dodoma, familia yake,ndugu jamaa na marafiki kwa kuondokewa na Dada yetu,Mwanafunzi Mwenzetu ukizingatia alibakiza miezi michache tu kuhitimu shahada yake ya Kwanza.
       Bwana Alitoa Na Bwana Ametwaa Jina La bwana Lihidimiwe.Amin.
                                        Imetolewa Na Lukaza Josephat
                                                LJ BLOG ADMINISTRATION.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages