Mwanamuziki Bora wa Kike 2010 na Mshindi wa Tuzo ya Wimbo Bora Afrika Mashariki Featuring Kidumu,kwenye Tuzo za Kili Awards 2010, Judith Wambura aka Lady JD ametupia kwenye blog yake....
Sikuweza kufika kwenye tuzo za Kili Music Awards kwa kuwa
sikupatiwamwaliko,niliogopa kuzamia.
Nadhani walinisahau.........Tehe tehe tehe
Hata mwakilishi wangu yoyote pia hakuwepo ila Shabiki mmoja
aliyewepo alinipokelea na kuniletea tuzo Nyumbani Lounge
La muhimu zaidi nashukuru sana Watanzania wote mlionipigia kura, sina cha kuwalipa zaidi ya Asante Nashukuru wote mnaoendelea kuamini kuhusu JayDeeTuko pamoja siku zote.
Pia Komando jide alionesha bahasha ambazo mtu akishinda uwa anapewa kama kiwakilishi cha tuzo izo..
Bahasha imeandikwa Mwimbaji Bora wa Kike, ambayo kwa kidhungu nadhani ni Best Female Vocalist. Tuzo hiyo alipewa mtu mwingine Linah wa THT.
Tuzo niliopewa mimi iliandikwa Female Artist of the Year ambayo ni Msanii Bora wa Kike wa Mwaka. Nadhani ubinaadam tu hapo umepita kama kuna fotauti na imani zitarekebishwa, kama yangu ina mpunga zaidi basi wataniongezea tu! Wink!!
Bahasha ya kwanza inanihusu nahakika ila ya pili ilioandikwa Best East African song sina hakika sana kama tunagawana na Kidum au kila mtu kapewa ya kwake???
Sina taarifa za undani, itabidi mzigo niuhifadhi nisijeanza kuutumbua mara naambiwa si zangu
Mwaka Flani hivi nakumbuka wimbo wa Anita niliofanya na Matonya ulipata kuwa Wimbo bora wa Mwaka zikatoka Trophies 2 na kila mtu akapata fungu la pesa kiasi.
Sijajua kama na kwa wimbo huu niliofanya na Kidum itakuwa hivyo au mwaka huu ni tofauti manake kila mwaka mambo huwa yanabadilika kwenye Tuzo hizi.

SOURCE: GONGAMIX
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)