Na Mwandishi Wetu
Jukwaa la Ukumbi maarufu wa Diamond Jubilee uliopo Upanga jijini Dar es Salaam linatarajiwa ‘kuwaka moto‘ leo kwa shoo kali za wasanii waalikwa wakati tukio la utolewaji wa Tuzo za Kili 2010/11 litakapochukua nafasi.
Habari kutoka kwa waandaaji wa ‘event’ hiyo ‘zinashoo’ kuwa licha ya kuwepo kwa burudani za wasanii nyota wa muziki wa Kizazi Kipya wa ndani na nje ya Bongo, kivutio kikubwa kitakuwa kwenye ‘kategori’ ya Prodyuza Bora wa mwaka kutokana na wakali waliopangwa kuwania tuzo hiyo.
Miongoni mwa wakali hao ni mshindi wa mwaka jana Lamar Niekamp ‘Lamar’ (pichani) (R113), Marco Chali (R116), Man Water (R 115), Bob Junior (R106) na Pancho Latino (R121) ambao wanatajwa kuleta homa kali kwa mashabiki wanaopiga kura kusaka mshindi.
Kwa kuwa muda bado upo, unachotakiwa kufanya ni kuendelea kupiga kura kwa unayeona anastahili ili kumfanya aibuke mshindi kwa kuandika ujumbe mfupi ukianza na neno Kili halafu namba yake ya ushiriki kisha tuma kwenda namba 15747.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)