GLOBAL NA CLOUDS MEDIA WAZINDUA TAMASHA LA UZALENDO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

GLOBAL NA CLOUDS MEDIA WAZINDUA TAMASHA LA UZALENDO

 
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers na Mwenyekiti wa Tamasha la Uzalendo, Eric Shigongo (wa pili kushoto) akibadilishana mawazo na Meneja wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba (wa kwanza kushoto) wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Uzalendo kwa wanahabari leo katika Ofisi za Global zilizopo Bamaga jijini Dar es Salaam. Tamasha hili limeandaliwa na kampuni ya Global Publishers ikishirikiana na Clouds Media Group na linatarajiwa kufanyika Jumamosi ya tarehe 26 Machi, 2011 katika Viwanja vya Biafra, Kinondoni Dar es Salaam kuanzia, saa 5:00 asubuhi hadi saa 12:30 jioni. Wengine pichani ni Mratibu wa Tamasha hilo Juma Mbizo (kwanza kulia).
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers na Mwenyekiti wa Tamasha la Uzalendo, Eric Shigongo akifafanua jambo kuhusu tamasha hilo mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani).
 
Meneja wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba nae akizungumzia tamasha hilo.
 
Mratibu wa Tamasha la Uzalendo, Juma Mbizo akielezea jinsi walivyojiandaa vyema kwa ajili ya tamasha.
 
Msanii mkongwe wa muziki wa  Reggae aishie nchini Marekani, Innocent Galinoma, akielezea jinsi wasanii watakavyoshiriki katika tamasha  hilo.
 
Msanii wa Bongo Fleva, Joseph Haule 'Profesa Jay' nae akitoa nasaha zake kuhusu tamasha hilo.
Raisi wa bendi ya Stono Mayiyasika, Malou Stonch (kushoto) akiwa na Mzee Yusuf wa Jahaz Modern Taarab.
 
Baadhi ya wanahabari na wasanii wakifuatilia kwa makini tukio la uzinduzi wa tamasha hilo.
 
Mhariri Kiongozi wa Championi, Saleh Ally (kushoto) akibadilishana mawazo na Meneja wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.
 
Mhariri Mtendaji wa Global, Richard Manyota (katikati) akiwa na 'kiongozi' Oscar Ndauka (wa kwanza kushoto) wakibadilishana mawazo na mwandishi Livingstone Nkoi.
 
Profesa Jay akiwa na baadhi ya wasanii waliohudhuria tukio hilo.
 
Wasanii pamoja na waandaaji wa tamasha wakiwa katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi huo.
 
Mratibu wa Tamasha la Uzalendo, Juma Mbizo (wa kwanza kushoto nyuma) akiwa katika picha ya pamoja na wasanii.
 
Kutoka kushoto ni: wasanii Ambwene Yesaya, Flora Mbasha, Profesa Jay na Mbasha katika picha ya pamoja.
 
Mratibu msaidizi wa tamasha akiwa amepozi na Mkurugenzi wa kundi la Jahazi Modern Taarab, Mzee Yusuf  (wa pili kushoto).

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages