Kanali Muammar Gaddafi amesema Libya itapigana "vita vya muda mrefu" baada ya nchi za Magharibi kushambulia majeshi yake kwa ndege kulinda maeneo yanayoshikiliwa na waasi.
Ndege ya kijeshi ikifyatua bomu kwenda Libya
Baada ya shambulio moja, miili ya watu 14 ilikuwa imezagaa karibi na gari la kijeshi lililoteketezwa nje ya mji unaodhibitiwa na waasi wa Benghazi, kufuatia mashambulio yaliyofanywa na ndege za kijeshi za Ufaransa, limeripoti shirik la habari la Reuters.
Ndege ya kijeshi ya Ufaransa ikielekea Libya
Mabomu ya kurusha kwa ndege yalilipua vituo visivyopungua 20 vya anga mjini Tripoli, na pia katika jiji la mashariki la Misrata, wamesema maafisa wa kijeshi wa upande wa magharibi.
Televisheni ya taifa ya Libya imeonesha picha za watu 150 waliojeruhiwa katika mashambulio hayo. Imesema watu 48 wameuawa.
Shambulio la anga Tripoli
Mwandishi wa BBC wa masuala ya ulinzi Jonathan Marcus anasema wanaoapnga mipango ya kibita wa majeshi ya umoja, watakuwa wakitazama picha za satelaiti kuona hasara waliyosababisha kwa majeshi ya anga ya Kanali gaddafi na pia kuona kama wanahitaji kufanya mashambulio zaidi.
Hali tete Libya
Mkazi mmoja wa Misrata ameiambia BBC kuwa majeshi yanayomuunga KanaliGaddafi yameanza mashambulio mapya siku ya Jumapili.
Muammar Gaddafi
Amesema majeshi ya Magharibi hayana haki ya kuishambulia Libya, ambayo haijawafanya lolote.
"Tutapigana sentimita kwa sentimima," amesema, huku picha ya ngumi ya dhahabu ikigonga ndege ya Marekani ikioneshwa.
Awali, alisema atafungua maghala ya silaha kwa ajili ya watu kuilinda Libya na kuelezea mashambulio hayo kama "vita viovu".
Saa za alfajiri siku ya Jumapili, milipuko ya mabomu ilitanda katika anga ya Tripoli na milipuko mingine kadhaa kusikika.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)