CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kuwa hakina nia, ajenda wala lengo la kuipindua serikali iliyoko madarakani kwa njia ya maandamano, bali hofu na woga alionao Rais Jakaya Kikwete na viongozi wengine inatokana na kushindwa kutekeleza ahadi na kuwajibika kwa wananchi. Kimesema kuwa pamoja na kuenezwa propaganda hiyo ya kupindua serikali, na nyingine kama za kuvuruga amani ya nchi, ukabila, udini na kufadhiliwa, hakitaacha kufanya kazi yake ya siasa ya kuiwajibisha serikali, kwa kusimamia hoja za wananchi juu ya mwenendo wa nchi na viongozi wao....soma zaidi. Kwa Habari Zaidi <<< BOFYA HAPA >>> |
-
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)