Viongozi wa Manispaa ya Kinondoni wakisikiliza maswali ya wanahabari baada ya kutoa ripoti hiyo. Kutoka kushoto ni RPC wa Kinondoni, Charles Kenyela, Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Lugimbana na kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Raphael Ndunguru.
HALMASHAURI ya Manispaa ya Kinondoni na Jeshi la Polisi wilayani humo leo wametoa ripoti kuhusu watoto wachanga 10 waliokutwa wamezikwa kaburi moja karibu na makaburi ya Mwananyamala kwa Kopa jijini Dar es Salaam.
Ripoti hiyo haikumtaja hata mzazi mmoja aliyekamatwa wala kujulikana ingawa uchunguzi wa polisi unaendelea. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Charles Kenyela, amesema mpaka sasa wamewakamata watu watatu ambao ni wafanyakazi wawili wa chumba cha kuhifadhia maiti wa Hospitali ya Mwananyamala, Said Ally Salum, Siraj Ally Mbuli na mlinzi wa Manispaa ya Kinondoni, Sofia Hassan Abdalah ‘Kandoro’.

Mwandishi wa Global Publishers, Makongoro Oging’ akiuliza maswali juu ya ripoti hiyo.
PICHA: RICHARD BUKOS /GPL
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)