Mchungaji Mwansasu alipokuwa akihubiri kanisani leo.
IKIWA ni siku moja tangu Rais Jakaya Kikwete avunje ukimya na kuzungumzia sakata la kampuni ya kufua umeme ya Dowans, baadhi ya viongozi wa dini mkoani Morogoro wameibuka na kuwataka waumini wapinge waziwazi kulipwa kwa deni la Dowans.
Agizo hilo la kuwataka Wakristo wote nchini wasikubali deni hilo lilitolewa na Mchungaji Mwansasu alipokuwa akihubiri leo asubuhi katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Mji Mpya mjini Morogoro kwenye ibada ya kwanza iliyofurika waumini.
"Nawaomba Wakristo wote mnaposikia habari za Dowans msikie maumivu mionyoni na kutambua uovu wa ufisadi ulivyo,” alisema mchungaji huyo mwalikwa ambaye kwa sasa anasoma katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokine mkoani hapa.
Pia mchungaji huyo aliwataka wanandoa wavumiliane katika ndoa zao wasiwe kama jiwe la barafu ambapo linapotoka kwenye raha ya baridi iliyopo kwenye friji huyeyuka.
"Ndoa nyingi siku hizi zimekuwa kama barafu, mwanamme akifilisika mwanamke anayeyuka na kutafuta mwanaume mwingine; na kwa mwanamme naye, mwanamke akiugua na kuchoka kwa umri, mumewe anatafuta mwanamke mwingine aliyenona,” alisema mchungaji.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)