WAZIRI WA AFYA KUPIGA KAZI NA WASANII WA KIZAZI KIPYA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WAZIRI WA AFYA KUPIGA KAZI NA WASANII WA KIZAZI KIPYA

Waziri wa Afya, Dk.Haji Mponda (pichani) ameahidi kupiga mzigo na mastaa 10 wa muziki wa Kizazi  Kipya  nchini, wanatambulika kama Mabalozi wa ‘Malaria No More’.

Akizungumza na Ijumaa ofisini kwake, Posta jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Mheshimiwa Mponda aliwataka mabalozi hao kutunga nyimbo za hamasa na kubadili tabia ya kuudharau  Ugonjwa wa Malaria iliyojengeka miongoni mwa watu.

Mponda aliwataka wasanii hao kutafuta njia mpya  za kusambaza ujumbe  kuhusu  kujikinga na ugonjwa huo. 

“Niko tayari kushirikiana nao, lakini nawaomba kutunga nyimbo zenye hamasa  na pia  kutafuta njia mbadala za kuhamasisha watu waelewe zaidi kuhusu ugonjwa huu, wakati mwingine unaweza kuona mtoto ana dalili zote za Malaria lakini mama yake anampa dawa za kutuliza maumivu kisha anaendelea na shughuli zake, hii ni kwa sababu ya uelewa mdogo,” alisema Mponda.

Wasanii waliopo katika programu hiyo ni Judith Wambura ‘Lady Jaydee’, Joseph Haule ‘Profesa Jay’, Mwasiti Almas, Amini Mwinyimkuu na Banana zorro.

Wengine ni Naseeb Abdul ‘Diamond’ Lawrence Marima, Barnaba Elias, Fareed Kubanda ‘Fid Q’ na Sunday Mangu ‘Linex’.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages