Ofisa Mtendaji wa Kata ya Doma, Wilaya ya Mvomero, Mkopi Seletine ( aliyekaa ) akiwaorodhesha baadhi ya wananchi 219 waliosainishwa vocha za pembejeo za ruzuku na Wakala wa Usambazaji wa Vocha hizo wa Kata ya Doma kwa kushirikiana na Kamati ya Vocha hizo ya Kijiji pamoja na Ofisa Mtendaji wa Serikali ya Kijiji, ili kuwa na kumbukumbu zitakazosaidia kupata mbolea na mbegu zao baada ya kuandaliwa utaratibu mwingine.
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, katika Mkoa wa Morogoro, Fatma Mwassa,( katikati)pamoja na Ofisa mmoja wa Wilaya hiyo wakivipitia vitabu vya vocha za ruzuku ya pembejeo za kilimo ya mbolea na mbegu , vilivyo' chakachuliwa'ufuatia wananchi 219 miongoni mwa 225 kusainishwa na kupewa sh: 10,000 bila kupewa pembejeo hizo hizo baada ya kurubuniwa na Wakala wa Usambazaji wa vocha Kata ya Doma aliyekula njama na Wajumbe wa kamati ya Kijiji ya vocha ya ruzuku kwa kushirikiana na Ofisa Mtendaji wa Kijiji na hivyo kuiibia Serikali mamilioni ya fedha, tukio lililotokea Desemba 31, 2010.Picha na Habari na Mdau John Nditi-TSN
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)