Mwanasiasa aliyejeruhiwa vibaya, Giffords.
WATU sita wameuawa, na mjumbe mwanamke wa Baraza la Congress la Marekani yuko mahututi baada ya kupigwa risasi na mtu mmoja huko Azirona, Marekani.
Shambulio hilo lilitokea nje ya duka kubwa la bidhaa huko Tucson ambako Gabrielle Giffords (40) mwanachama chama cha Democratic ambaye ni mjumbe wa Baraza la Congress, alikuwa akikutana na watu wa jimbo lake.
Miongoni mwa waliokufa alikuwa ni jaji wa shirikisho, John Roll na mtoto wa kike mwenye umri wa miaka tisa.
Afisa mmoja wa zimamoto wa Tucson alisema watu sita waliuawa na 13 kujeruhiwa katika shambulio hilo.
Mtuhumiwa wa shambulio hilo aliyejulikana kama Jared Lee Loughner (22) alianza kufyatua risasi akiwa karibu kwa kutumia bastola yake.
Ofisa mkuu wa eneo hilo, Sheriff Clarence Dupnik, alisema mtuhumiwa huyo ambaye alitiwa mbaroni baada ya shambulio hilo “alikuwa na matatizo ya siku nyingi”.
Sheriff huyo aliwaambia waandishi wa habari kwamba wanamtafuta mwanamme wa pili ambaye anahusiana pia na tukio hilo.

Picha tofauti za mtuhumiwa Jared Loughner.
Kufuatia tukio hilo, Giffords alikimbizwa kwa ndege hadi Tucson ambako alifanyiwa upasuaji ambapo mmoja wa madaktari waliokuwa wakimpa tiba alisema alikuwa na matumaini kwamba atapata afueni.
Katika shambulio hilo, risasi ilipita moja kwa moja katika ubongo wa mwanamke huyo.
Akizungumzia tukio hilo, Rais Barack Obama wa Marekani alisema: “Hatujui nini kilisababisha tendo hilo la kinyama.”
Pamoja na kauli yake hiyo, shirika la habari la Sky la Marekani limesema rais huyo amemtuma mkurugenzi wa shirika la upelelezi la nchi hiyo (FBI), Robert Muellter, kwenda Arizona kusimamia uchunguzi wa tukio hilo.
Mauaji ya kutumia bunduki nchini Marekani ni ya kawaida ambapo wakati mwingine huhusisha mauaji ya watu wengi, lakini mauaji ya wanasiasa ni jambo adimu.
Shambulio hilo limefuatia uchaguzi wa utata wa wajumbe wa baraza la Congress uliofanyika mwezi Novemba mwaka jana ambapo chama cha Democratic kilikuwa kimelenga kuubadili mfumo wa huduma za afya nchini humo na mabadiliko katika mfumo wa uhamiaji wa watu kuingia nchini humo.
Mnamo mwezi Machi mwaka jana, dirisha la ofisi ya Giffords lilivunjwa baada ya Baraza la Congress kupitisha mabadiliko ya huduma za tiba, jambo ambalo wafuasi wa chama cha Republican walikuwa wanalipinga.

Eneo lilipotokea tukio hilo.
Mtuhumiwa alitokea nyuma ya mwanasiasa huyo ambapo alifyatua risasi zaidi ya 20 kwa mama huyo na watu wengine waliokuwa katika mkusanyiko huo.
Mama huyo anayechipukia katika siasa, ni mmoja wa wanachama wa Democratic Party walioweza kuhimili vishindo vya chama cha Republican katika eneo hilo uchaguzi uliopita mwaka jana.

Kwa Msaada Wa Mtandao.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)