SAMWEL SITTA: DOWANS NI YA WAJANJA WALIOFANYA UJANJA KWENYE KARATASI NA SERIKALI KUINGIA MKENGE - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

SAMWEL SITTA: DOWANS NI YA WAJANJA WALIOFANYA UJANJA KWENYE KARATASI NA SERIKALI KUINGIA MKENGE

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta
-----


 KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida Waziri katika Baraza la Mawaziri ameamua kumkosoa mwenzake hadharani kutokana na uamuzi alioutangaza hivi karibuni kwa Taifa.

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ndiye amepata ujasiri huo kwa kumkosoa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, kutokana na kutangaza kuilipa Kampuni ya kufua umeme ya Dowans Sh bilioni 94, hatua ambayo anaona hakustahili

kuitangaza yeye.

Sitta alisema hayo jana, baada ya kumaliza kuongoza mahafali ya Shule ya Sekondari ya Dini ya Maranatha iliyoko Mianzini Kata ya Kaloleni jijini hapa.


Alisisitiza kuwa Dowans ni ya wajanja waliocheza ujanja kwenye karatasi na Serikali kuingia

‘mkenge’ kulipa kitu ambacho alikielezea kuwa hakina sababu za msingi.

Waziri huyo alisema Kampuni ya Richmond iligundulika na Kamati ya Uchunguzi ya Bunge iliyoongozwa na Dk. Harrison Mwakyembe, kuwa haikuwa halali lakini inasikitisha kuona na kusikia mbia wake, Dowans amehalalishwa, “kitu hicho ni hatari sana kufanywa na jamii itakuja kutuhukumu kwa hilo.


‘’Mzabuni feki anacheza karata zake na mbia wake Dowans nasi tudiriki kulipa kitu ambacho si halali … kamwe haiwezi kuwa halali katika maisha yote,” alisema.


Sitta alitoa mfano wa mtu ambaye hakumtaja jina, kuwa ana kampuni 17 nchini, lakini jina lake halionekani katika kampuni yoyote na ambaye alidai anacheza michezo michafu na kulipwa mamilioni ya fedha.


Alisema watu hao wapo na wanacheza na karatasi na kuhalalisha kujipatia mamilioni ya fedha za walipa kodi wa nchi hii.


Pia Waziri alisikitishwa na kauli ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya ‘kunawa mikono’ mapema na kukubali kuilipa Dowans, hatua ambayo alisema ilimshitua sana.


Alisema kwa jambo zito kama hilo, ni lazima Serikali ingekaa chini na kuliangalia kwa mapana na hata ingewezekana kuitisha kikao cha Baraza la Mawaziri kujadili suala hilo kwa kina na kulipatia ufumbuzi wa pamoja, lakini Waziri Ngeleja amelisema haraka jambo hilo.


Sitta alisema Sh bilioni 94 zingejenga barabara ya lami ya kilometa 100 yenye ubora wa hali ya juu vilevile kwa kujenga shule za sekondari 300 za kidato cha kwanza hadi cha nne.


‘’Naweza kusema wajanja wametuzidi akili na wamefaidi kodi za wananchi kujilipa, lakini elimu bila maadili nchi inaweza kwenda mrama,’’ alisema.


Waziri Sitta alisema kwa sasa huwezi kufanya lolote juu ya malipo ya Dowans kwani ‘’unawezaje kufunga zizi la ng’ombe wakati ng’ombe wote wameshaondoka?’’


Alisema ataendelea kusema ukweli mwanzo hadi mwisho bila kumwogopa mtu na kamwe hawezi kuwa mwongo na mnafiki kwa jambo lolote.


Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi (ICC) iliamua katika hukumu yake Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) iilipe Dowans fidia ya Sh bilioni 94 kutokana na Tanesco kuvunja mkataba nayo.


Uamuzi huo uliridhiwa na Serikali baada ya Mwanasheria wake Mkuu, Frederick Werema kuipitia hukumu hiyo na kujiridhisha kuwa ni halali.

 -
imeadikwa na John Mhala

3 comments:

  1. MKINGA OSWIN.10:51 PM

    ANKAL LUKAZA, BIG UP SANA, KAZI YAKO NIKUBWA SANA MBELE YA WATZ SISI. UCRUDI NYUMA, ENDELEA KUKANYAGA UMANDE VIZURI HAPO UDOM ILI UIWEKE JAMII KARIBU NA DUNIA. WEWE NI MKALI KAKA.

    I MUST DO SOMETHING WITH YOU.

    ReplyDelete
  2. MKINGA, OSWIN.10:53 PM

    PIA NAKUSHAURI, TUMIA MAKUSANYIKO NA MAKONGAMANO MBALIMBALI KUITANGAZA, NAMI PIA KAMA MDAU WAKO NA KAZA BUTI, KUKUPELEKA MBELE. MENGINE TUTAONGEA FACE TO FACE.

    ReplyDelete
  3. MKINGA10:55 PM

    KAULI YA WAZIRI SITTA, IZINGATIWE. KUMBE HUYU SITTA BADO NI MWIBA MKALI...!!!??? NILIDHANI ATAPOA BAADA YA KUMRICHMUNDI USPIKA...????

    HUYU JAMAA NI KICHWA SANA, NAAMINI AFRIKA MASHARIKI KUNA WAZIRI C YULE.....

    ReplyDelete

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages