Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Dar es Salaam, Meneja wa bia ya Safari Lager, Fimbo Butala (Pichani, kushoto)aliyataja majina hayo kuwa ni Mercy Shayo wa Bomang'ombe mkoani Kilimanjaro na wakazi wa Dar es Salaam, Paul Luvinga wa Sinza na Leonard Mtepa wa Mwanayamala.
-----------
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager imetangaza majina matatu ya waliofanikiwa kuingia fainali za shindano la tuzo ya 'Shujaa wa Safari Lager', ambalo mshindi atajinyakulia kitita cha sh. milioni 7.
Mbali ya kunyakua kitita hicho, mshindi atapatiwa pia sh. milioni 3, kwa ajili ya ujenzi wa mradi wowote wa kijamii ikiwemo ya maji, elimu na afya katika eneo anamoishi, huku walioingia fainali wote wawili wakipata sh. milioni moja kila mmoja kama kifuta jasho.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Dar es Salaam, Meneja wa bia ya Safari Lager, Fimbo Butala aliyataja majina hayo kuwa ni Mercy Shayo wa Bomang'ombe mkoani Kilimanjaro na wakazi wa Dar es Salaam, Paul Luvinga wa Sinza na Leonard Mtepa wa Mwanayamala.
Butala alisema, baada ya kupokea mapendekezo mengi toka kwa wananchi wakipendekeza mashujaa wao na mambo waliyofanya kwa jamii, kazi iliyofuata ilikuwa ni kupitia na kuchambua mapendekezo hayo kwa kuangalia vigezo muhimu, ili kuweza kupata majina hayo matatu.
Alisema kufuatia kupatikana washimdani hao sasa TBL itachapisha mambo aliyofanya mashujaa hao watatu katika magazeti, televisheni na redio ili wananchi wote waelewe na kisha waweze kupiga kura kumchagua shujaa wanaetaka atwae tuzo hiyo ya 'Shujaa wa Safari Lager 2010'.
Kuhusu utaratibu wa kupiga kura, Butala alisema, baada ya kufuatilia mambo waliyofanya mashujaa hao walioingia fainali, wananchi watatakiwa kumpigia kura kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno kuanzia jana jana, na upigaji kura utaendelea hadi Januari 21, mwaka huu siku ya fainali.
Alisema watakaopenda kuhsiriki kupiga kura wataingia katika sehemu ya ujumbe katika simu zao na kuandika neno 'Shujaa' kisha wataacha nafasi na kuandika herufi inayomwakilisha shujaa husina ambapo Mercy ni A, B kwa Luvinga na C kwa Mtepa, kisha watatuma kwenda namba 15310 na baada ya muda mhusika atapata ujumbe kukuthibitishia kuwa kura yake imepokewa.
Tuzo ya shujaa wa Safari Lager ilizinduliwa rasmi tarehe 24 Novemba 2010, ikiwa na lengo la kutambua na kuheshimu watu wanaofanya mambo makubwa yanayoleta mabadiliko kwa jamii inayowazunguka, bila kusukumwa na uwezo wa pesa wala madaraka waliyonayo.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)