RAISI JAKAYA KIKWETE AWATULIZA CHADEMA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

RAISI JAKAYA KIKWETE AWATULIZA CHADEMA


Waandishi Wetu
SIKU moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kutangaza kuunda tume itakayoratibu mjadala wa kuandika katiba mpya,wanasiasa na wasomi wameonyesha  kuridhishwa, huku Chadema wakitahadharisha kuwa hatua hiyo iwe kwa maslahi ya wengi. Vile vile, CUF nao wamempongeza na kumwonya Rais Kikwete kuwa makini na watendaji wake wenye msimamo wa kihafidhina kwamba asipokuwa makini wanaweza kumwangusha.

Chadema kupitia Katibu mkuu wake, Dk Wilibrod Slaa na Mwasisi wa chama hicho, Edwin Mtei wamempongeza Rais Kikwete kwa uamuzi huo wakitaka katiba hiyo ilenge kuwanufaisha wananchi wote.
 Mtei ambaye pia ni Mwenyekiti mstaafu wa chama hicho, aliiambia Mwananchi Jumapili jana kuwa wamefurahishwa na rais kuamua kuunda tume ya kuratibu uanzishwaji wa katiba mpya kwa vile hicho ndicho walichokuwa wakikipigania siku zote.Alisema chama chake kitatoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha kuwa mchakato wa uundwaji wa katiba hiyo unatekelezwa kwa nia njema.

"Kwanza naomba kumshukuru Mungu kwa kumpa mawazo mazuri rais, lakini sasa nadhani watawala wetu wametambua ya kuwa zile kelele za madai ya katiba mpya tulizokuwa tukizitoa zinasikilizwa," alisema.

Dk Slaa kwa upande wake alisema rais amekosea kwani hajasikiliza kilio cha wananchi,kwa sababu wananchi hawataki ipelekwe kujadiliwa Ikulu kwa kuundiwa kamati.

"Hapa kilio cha wananchi hakikusikilizwa kabisa kwa sababu Tanzania inataka katiba iliyotengezwa na wananchi sio serikali kuunda kamati," alisema.Alionya kuwa suala la katiba kuundiwa kamati ya kuratibu inaonyesha kabisa kuwa katiba hiyo itakuwa ni ya serikali na sio ya wananchi.
Novemba mwaka jana wabunge wa Chadema walisusia hotuba ya Rais Kikwete bungeni mjini Dodoma wakipinga mchakato wa matokeo ya kura yaliyompa urais kwamba hayakuwa halali na kuanzisha mkakati wa kudai kuandikwa kwa katiba mpya.

 Hatua ilisababisha wabunge wa chama hicho kugawanyika na wengine kutuhumiwa kwamba walikihujumu chama  hicho kwa kushindwa kushiriki kususia hotuba ya rais.
Kwa Taarifa Zaidi  BOFYA HAPA
Source: Mwananchi Newspaper.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages