NEWS ALERT: WANAFUNZI WA UDOM KITIVO CHA SAYANSI YA JAMII NA LUGHA WAKUSANYIKA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

NEWS ALERT: WANAFUNZI WA UDOM KITIVO CHA SAYANSI YA JAMII NA LUGHA WAKUSANYIKA

Wanafunzi Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Kitivo Cha Sayansi Ya Jamii Na Lugha Wakusanyika Kusikiliza Maelekezo Kutoka Kwa Raisi Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Kitivo Cha Sayansi Na Lugha Mh Leornad Singo Kuhusu hatma ya Wahadhiri Wa Chuoni hapa Ambao Wamegoma tokea Jumatatu mpaka Leo lakini wenyewe wahadhiri wanasema wapo kwenye Extended Meeting.Kitu ambacho kinawaathiri Wanafunzi kwa wahadhiri hao kutoingia Katika Vipindi.Wanafunzi Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Hawakuingia Darasani Tokea Jumatatu mpaka Leo.

Wanafunzi Wakiwa Makini Kusikiliza Maelekezo yanayohusu Mustakabadhi Wa Maisha yao Ya Kitaaluma mara baada ya kutoingia Darasani Takribani wiki moja sasa.Kwa taarifa ambazo wanafunzi wamepewa na Raisi Wa Kitivo Chao Mh Leornad Singo Kwamba Kesho Ijumaa Baadhi Ya Makatibu Wa Kuu Wa Wizara Baadhi Watakua Hapa Chuo na Mkaguzi Mkuu Wa Hesabu Za Serikali (CAG) ili Kukagua Mapato Na Matumizi Ya ChuoNa Kuwasilisha Ripoti Yao Kwa Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda Ambae anatarajia Kuja Udom Jumamosi Kwaajili Ya Kutatua Matatizo Ya Wahadhiri Na Wanafunzi Kwa Ujumla.
 Wanafunzi Wakiwa Makini Kusikiliza Maelekezo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages