Na Mwandishi Wetu
Watanzania sita, wakiwemo wasanii wawili wa maigizo, wamefungwa Magereza mawili ya Hong Kong nchini China baada ya mahakama kuwakuta na hatia ya kujihusisha na biashara ya ukahaba, Ijumaa linakuwa la kwanza kukujuza.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha uhakika, wabongo hao, wamefungwa kwenye Magereza ya Lai Chi Kok na Tuemun ambayo ni maalum kwa wafungwa wanawake.
Watanzania hao, ambao wanatumikia kifungo cha wiki sita gerezani ni Jack aliyewahi kuwa Muigizaji wa Kundi la Sanaa la Kidedea akijulikana kwa jina la Safina, Maua ambaye naye amewahi kuwa msanii wa maigizo (kundi halijajulikana) na Tina Mkongo aliye maarufu kwenye Club za Jolly na Ambiance za jijini Dar.
“Jack ni yule Safina ‘alikuwaga’ Kidedea, tena hivi karibuni tu amecheza filamu ya ‘Inye’, msanii mwingine anaitwa Maua, huyu sijui alikuwa kundi gani, na hao wengine niliokutajia,” kilisema chanzo kimoja.

Kwa Taarifa Zaidi BOFYA HAPA
Source: GLOBAL PUBLISHER TANZANIA
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)