HABARI PICHA NA: DUNSTAN SHEKIDELE,MOROGORO
Ajali ya funga mwaka imetokea jana (Desemba 31) katika daraja la Wami, Barabara Kuu ya Chalinze Segera baada ya lori kufeli breki wakati likishuka mlima uliyopo jirani na daraja hilo na kupinduka. Watu walioshuhudia tukio hilo waliueleza mtandao huu kwamba dereva wa gari hilo aina ya Leyland lililokuwa likitokea upande wa Chalinze, alifanya jitihata za kutaka kuepusha ajali hiyo lakini kutokana na mteremko mkali ulioambatana na kona kali, alishindwa kukwepa. Watu wote waliokuwemo kwenye lori hilo lililokuwa limebeba shehena ya sukari gulu, walifariki dunia huku baadhi ya maiti zikiwa zimebanwa na roli hilo. Kufuatia ajali hiyo, magari mengi yalikwama kutumia barabara hiyo kwa zaidi ya saa mbili.
Hello LJ
ReplyDeleteHeri ya mwaka mpya.
Nimepita hapa baada ya kuona maoni yako mahala. Nikajua utakuwa na blog na nikapita. Nimefurahishwa na mambo mchanganyiko, muonekano wake na haswa ukweli kwamba unatoa CREDITS za sources za habari na picha zako.
Nuff RASpect kwako na nimeweza pata transcript ya hotuba ya Rais ambayo nimeitumia sasa katika post yangu. Pia picha
Blessings Man.
PamoJAH