MICHAEL MOMBURI
ELAN club de Mistudje ya Comoro inaendelea na mazoezi makali mjini Moroni, lakini majina ya wachezaji watatu wa Simba yamenaswa na klabu hiyo.
Simba na Elan zinakwaana katika mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika Januari 29 mjini Moroni na tayari mabingwa hao wa Comoro wameanza mazoezi huku habari za ndani zikieleza kuwa uongozi wao umetenga fungu la kutosha kwa kampeni hizo na tayari wamepata baadhi ya maelezo muhimu ya wachezaji wa Simba na aina ya uchezaji wake.
Wachezaji wa Simba wanaozungumzwa zaidi na kufahamika miongoni mwa wachezaji wa Elan ni Mussa Hassan Mgosi, Juma Kaseja na Mohammed Banka ambao ni mastaa wa kikosi cha kwanza cha Simba.
"Hapa Elan wanaendelea na mazoezi yao ukijaribu kuwauliza wachezaji wanawafahamu zaidi ni wachezaji watatu wa Simba ambao ni Mussa Mgosi, Juma Kaseja na Mohammed Banka," Eli-Juma Din, mmoja wa waandishi wa michezo wa Comoro ambaye anafuatilia mazoezi ya Elan aliiambia Mwanaspoti jana Ijumaa kwa simu.
Alisema kuwa hata mfumo wa uchezaji wa Simba umefahamika na sasa Elan inafanya mazoezi kuhakikisha wanadhiti mchezo wa Simba.
"Elan wamejiandaa vizuri na wanasapoti kutoka kwa mashabiki na viongozi wao, nimekuwa nawafuatilia kwa karibu wanaonekana wana morali na imani kubwa ya kufanya vizuri safari hii kwenye michuano ya kimataifa, hawana hofu ingawa Simba inazungumzwa kama klabu imara,"aliongeza mwandishi huyo na kudai kuwa Elan imesajili wachezaji wengi vijana.
Rais wa timu hiyo, Hamidou Ranfiou Sambaouma ametangaza kuwa; "Tulistahili ubingwa wa nchi na tutakachofanya sasa ni kuzama kwenye pochi kuhakikisha kwamba tunaweka mazingira mazuri zaidi ya kusonga mbele kwenye haya mashindano ya kimataifa."
Kaseja na Mgosi kwa nyakati tofauti wameitamkia Mwanaspoti kuwa hawana wasiwasi na Elan lakini hataidharau kwavile timu za Comoro zimekuwa zikiondoshwa kwa idadi kubwa ya mabao kila mara.
Simba imepanga kuondoka Dar es Salaam Januari 26 ili kuzoea hali ya hewa ya Comoro siku chache kabla ya mchezo huo muhimu ambao wakiitoa timu hiyo wanakwaana na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Kocha wa Simba, Patrick Phiri aliliambia Mwanaspoti kuwa Elan ina wachezaji kadhaa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Comoro ambacho hivi karibuni kilipata kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa Zambia kwenye mchezo wa kufuzu Mataifa ya Afrika 2012.

Source:Mwanaspoti Newspaper.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)