Jeshi la Polisi Mkoani Arusha Latawanya Maandamano ya Chadema Leo - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Jeshi la Polisi Mkoani Arusha Latawanya Maandamano ya Chadema Leo

 

 Viongozi wa juu wa CHADEMA, wakiongowa na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe (Watano kulia) na katibu mku, Dk.Wilbroad Slaa(Wasita kulia) wakiongoza maandamano yaliopigwa marufuku na polisi jana mjini Arusha.Hatimaye polisi iliwatolea uvivu na kuwapiga kwa mabomu ya machozi. Habari zaidi zaeleza kuwa Mbowe anashikiliwa na polisi. 
Maandamano ya wanaosadikiwa kuwa wanachama na wapenzi wa CHADEMA yakikatisha mitaa ya jiji la Arusha muda mfupi uliopita
 Maandamano yakiwa yamepigwa stop
Maandamano yakiwa yamepigwa stop Maeneo ya unga limited
Arusha hapatoshi dakika hii.
Mke wa Katibu Mkuu wa Chama cha CHADEMA Dk.Wilbroad Slaa, Josephine akiwa ametapakaa damu baada ya kujeruhiwa vibaya kwa kipigo na polisi wakati wakivunja maandamano ya viongozi na wanachama wa chama hicho yaliyofanyika mjini Arusha jana.Katika maandamano hayo watu kadhaa walijeruhiwa baada ya kupigwa na pilisi wa kutuliza ghasia.
MWENYEKITI WA CHADEMA NA MBUNGE WA HAI MH. FREEMAN MBOWE NI MIONGONI MWA VIONGOZI KADHAA WA CHAMA HICHO AMBAO WAKO MIKONONI MWA POLISI JIJINI ARUSHA DAKIKA HII, BAADA YA KUTIWA MBARONI KWA KILE KILICHOONEKANA KUWA MAANDAMANO BATILI.

TIMU YA GLOBU YA JAMII AMBAYO IKO ENEO LA TUKIO LIMEWATAJA VIONGOZI WENGINE WALIO KOROKORONI KUWA NI MBUNGE WA ARUSHA MJINI MH. GODBLESS LEMA, MBUNGE WA ROMBO MH. JOSEPH SELASINI NA WANACHAMA WENGINE KADHAA WA CHADEMA.

HABARI ZINASEMA POLISI WALITAWANYA MAANDAMANO HAYO YALIPOKARIBIA OFISI ZA TAKUKURU NA KWAMBA BAADA YA VUTA NIKUVUTE, MH. MBOWE NA WENZIE WAKAKAMATWA NA KUTUPWA RUMANDE.

AIDHA HABARI ZINADATISHA KWAMBA JIJI LA ARUSHA LINARINDIMA KWA MPAMBANO WA KUKIMBIZANA WA POLISI NA MAKUNDI YA WATU WANAODAIWA KUTAKA KWENDA KITUO CHA POLISI KUWATOA WALIOKAMATWA KWA NGUVU.
Picha kwa msaada wa Mdau Paul Sarwatt ,Khalfan Said na Aravind BK

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages