MAUAJI ya kinyama yamezidi kutishia maisha ya wakazi wa Manispaa ya Iringa baada mfanyakazi mmoja wa kituo cha kuziba pacha za magari katika eneo la Mshindo mjini hapa, Nico Chalale (28), kukutwa amekufa kifo cha mashaka kwa kunyongwa shingo usiku wa kuamkia Sikukuu ya Krismasi, ikiwa ni siku moja baada ya kuchinjwa mfanyabiashara wa samaki, Bukuri Mvulla na watu wasiofahamika jirani kabisa na eneo hilo.
Kijana huyo alikutwa akiwa amefungwa kamba shingoni huku akiwa amepiga magoti hali inayozua maswali zaidi kwa wakazi wa mjini Iringa na kuingiwa na hofu ya kuwepo kwa mtandao wa watu wanaojihusisha na mauaji hayo.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi wiki iliyopita, wakazi wa eneo la Mshindo, mjini Iringa walisema kuwa kifo cha fundi huyo ambaye mwili wake ulikutwa eneo la kazini kwake unawafanya kuingiwa na hofu na wameliomba jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina dhidi ya mauaji hayo.
Wananchi hao walisema kuwa inasikitisha na kutishia uhai wao kuona watu wakiendelea kunyongwa na kuuawa kinyama katikati kabisa na mji huo wa Iringa.
”Kifo cha Chalale ni tukio la tatu kutokea ndani ya kipindi kifupi cha wiki mbili ambapo tukio la kwanza lilikuwa la aliyekuwa kamanda wa kampuni ya ulinzi binafsi ya Force Group marehemu Charles Tulo ambaye alikutwa amejinyonga katika mti mfupi unaokisiwa kuwa na futi kama tatu wakati yeye ana urefu wa fupi 5, lazima kuna wauaji hapa,” alisema mwananchi mmoja kwa sharti la kutoandikwa jina gazetini kwa sababu za kiusalama .

Hata hivyo, alisema mauaji hao hayakuishia hapo kwani siku moja kabla ya Krismasi mfanyabiashara wa samaki Mvulla alikutwa akiwa amechinjwa shingo kama kuku na mwili wake kutelekezwa ndani ya daladala mbovu.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Evarist Mangalla ametihibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa wanaendelea kufanya uchunguzi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Evarist Mangalla ametihibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa wanaendelea kufanya uchunguzi.
Kwa Msaada Wa Global Publisher Tanzania
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)