WATANZANIA TUNAWAOMBA KUMPIGIA KURA DIAMOND - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WATANZANIA TUNAWAOMBA KUMPIGIA KURA DIAMOND

Msanii Diamond akila pozi na kupewa changamoto kutoka kwa Queen wa Pop ambaye alikuwa  mshindi wa MTV Award Miaka ya Nyuma Britney Spears mjini London baada ya Urban Tour-----
 Salaam,

URBAN PULSE CREATIVE Inawaomba na kuwasihi watanzania wote pale walipo kuwa wazalendo na kumpigia kura Mtanzania mwenzetu, Ndugu Yetu, rafiki Yetu, Msanii wetu mpendwa Diamond ambaye amebahatika kuwa miongoni mwa wasanii wachache waliochaguliwa kuwania Tuzo za MTV MAMA AFRICA Awards Zitakazo fanyika Nigeria Jijini Lagos Jumamosi hii 11.12.10

 Hivyo Basi watanzania na wadau wote wa muziki mnaombwa sana kupiga kura ili Kumwenzesha Diamond ashinde tuzo hii muhimu iweze kuja Tanzania ili kuiwezesha Nchi yetu kujulikana zaidi ulimwenguni na pia kuleta HESHIMA kubwa kwa kila MTANZANIA.

Namna ya kupiga Kura ni kama ifuatavyo:
1. Kwa njia ya simu unaweza kupiga kura yako kwa kuandika neno BNA DIAMOND kisha tuma  text kwenda namba 6262, kwa walio  nje yaTanzani tuma  text 15726.

2. Kutumia Mtandao  tembelea tovuti hii http://www.mtvbase.com/splash/mama/ bonyeza mtv mama halafu ingia ndani ya nominees  tunaomba umpigie kura as the best New Act.

Tafadhari fanya sehemu yako pia mwambie na mwenzako.
Asanteni sana Mungu awabariki.

Diamond Platinumz
akishirikiana na
URBAN PULSE CREATIVE

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages