Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Power Pool East Africa, Machwa Kagoswe, akitoa maelezo kwa Naibu waziri wa Viwanda na Biashara, Lazaro Nyalandu (katikati)kuhusiana na eneo litakalotumika kuzalishia umeme wa upepo mkoani Singida juzi. Serikali imeingia ubia kupitia Shiriaka la Maendeleo la Taifa (NDC) na kampuni binafsi ya Power Pool East Aftrica ili kuzalisha umeme huo kuanzia mwakani
.................................................................
Mpoki Bukuku
Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), limeingia ubia na Kampuni ya Power Pool East Africa kuzalisha umeme wa upepo mkoani Singida utakaogharimu zaidi ya Sh180 bilioni.
Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Lazaro Nyalandu, alisema tayari makubaliano yamesainiwa na NDC na kwamba, serikali itakuwa ikimiliki asilimia 51 ya hisa na nyingine zitakuwa za mwekezaji.Nyalandu alisema mradi huo utakuwa wa gharama nafuu katika uzalishaji utaingizwa kwenye gridi ya taifa na kwamba, kwa kuanzia zitazalishwa megawati 50 na baadaye zitaongezwa kulingana na uwezo wa wabia hao.
“Tokea kuanza kufungwa kwa mitambo, itachukua takriban miezi 15 ili umeme uingie gridi na hii itakuwa ufumbuzi wa matatizo ya umeme kwa sasa,” alisema Nyalandu.
Waziri huyo alisema katika makubaliano hayo, serikali itakuwa ikimiliki hisa za asilimia 51, nyingine zitabaki kwa mwekezaji binafsi na ujenzi unatarajia kuanza muda wowote.
Mkurugenzi wa Viwanda wa NDC, Alley Mwakibolwa, alisema ujenzi wa mitambo ya kutumia upepo kutasaidia kuzalisha umeme mapema, kwani mitambo ya aina hiyo huchukua muda mfupi kuwekwa ikilinganishwa na ile ya maji au gesi.
Kwa Taarifa zaidi BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)