Rais Jakaya Kikwete Ateua Wabunge Wapya Watatu Zakhia Meghji na Shamsi Vuai Nahodha Waula
Ndugu Shamsi Vuai Nahodha Zakia Hamdan Meghji
------------- TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete,amefanya uteuzi wa Wabunge watatu(3)kwa mujibu wa Ibara ya 66 (1)(e)ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, kama ilivyorekebishwa na kupewa mamlaka ya kuteua Wabunge 10.
Wabunge walioteuliwa ni Ndugu Shamsi Vuai Nahodha,Prof.Makame Mnyaa Mbarawa na Ndugu Zakia Hamdan Meghji.
Rais atateua wengine waliosalia siku zijazo.
Rais Kikwete ameshawasilisha majina ya wateule hao kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Anne Semamba Makinda(Mb)kwa ajili ya hatua zipasazo.
MWISHO
Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu.
Dodoma
17 Novemba, 2010
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)