WASTAAFU wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki jana walizua kizaa nje ya viwanja vya Mahakama Kuu, jijini Dar es Salaam baada ya kufunga barabara ya Kivukoni Front kwa kukaa na kulala katikati ya barabara hiyo kwa saa saba.
Wastaafu hao walichukua hatua hiyo kupinga uamuzi wa Jaji Njengafibili Mwaikugile wa Mahakama Kuu aliyekuwa akisikiliza kesi yao ya madai dhidi ya serikali kujitoa.
Kabla ya tafrani hiyo ya jana, wastaafu hao walifika mahakamani hapo kwa kile walichokiita kuwa ni kupewa hati ya malipo, lakini kinyume na matarajio yao Jaji Mwaikugile alitangaza kujitoa katika kesi hiyo.
Jaji Mwaikugile alisema ameamua kujitoa katika kesi hiyo baada ya kuona kwamba, kwa sasa hayuko katika nafasi nzuri ya kutenda haki kwa vile amebaini kuwa ana maslahi katika kesi hiyo, jambo ambalo kisheria anaruhusiwa kuchukua uamuzi huo.
Hata hivyo, wazee hao ambao walikuwa wakisubiri uamuzi wa suala lao nje ya mahakama, walipopewa taarifa za jaji kujiondoa katika kesi hiyo walilipuka kwa kelele za jazba kupinga uamuzi huo kwa madai kuwa ni kuwanyima haki yao ambayo wameisotea kwa miaka 34 sasa.
Katika kupinga uamuzi huo, baadhi ya wastaafu hao walimwaga machozi na kuamua kufunga barabara hiyo kwa kukaa na wengine kulala katikati ya barabara huku wakidai kuwa hawaondoki hadi haki yao ipatikane.
Hatua hiyo ilisababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa barabara hiyo hususani wenye magari kwani walilazimika kugeuzi ama kwa hiyari yao wenyewe au kuwa kulazimishwa na wastaafu hao kurudi walikotokea.
Hali hiyo pia ilisababisha usumbufu kwa shughuli za mahakama hiyo jambo ambalo lilisababisha geti la mbele la lango kubwa la kuingilia mahakamani hapo kufungwa kwa kufuli pamoja na mlango wa kuningilia ndani ya mahakama hiyo.
Wafanyakazi wa mahakama na watu wote waliokuwa wakifika mahakamani hapo walilazimika kuingilia mlango unaotumiwa na majaji.
Katika kupinga uamuzi wa Jaji Mwaikugile kujitoa baadhi ya wastaafu hao walisema:
Asha Juma:Hapa hatuondoki mpaka kieleweke, kajitoa nini, sisi tunataka atugee hela zetu kwani wenzetu Kenya walishalipwa. Kama kutuua mtuue tu.
Abdallah Hamis : Jaji hawezi kujitoa leo, maana yake nini? Tuueni tu na leo ndio siku yetu ya kufa hapahapa.
Salma Seif: Mume wangu ndiye mstaafu na sasa yuko hoi kitandani. Tumefiwa na watoto wetu wote. Mimi sina msaada wa kitu chochote na hali yangu ndio hii, tunaomba serikali itusaidie.
Chiku Lweso: Huyo Jaji kwa nini hakujitoa zamani leo ndio aje ajitoe? Serikali yetu inatunyanyasa, leo hatuondoki mpaka kieleweke.
Saida Hussein: Tumefiwa na watoto wetu wote na tumebaki na wajukuu tu tu nitafanyaje mimi huku akilia machozi.
Ladslaus Joseph: Tumevumilia vya kutosha kwani sasa ni miaka 34 tunaendesha kesi hii. Utawala wa sheria hapa haupo. Mahakamani hatuondoki tupigeni mabomu tu tufe.
Fatuma Mwinyi: Kama jaji kashindwa tunamtaka Kikwete kwa kuwa yeye ndiye mwenye uamuzi wa mwisho. Hapa sisi leo hatuondoki kama kufa tufe tu kwani tunateseka na maisha.
Ilipofika saa 7:00 wastaafu hao walifanya ibada katikati ya barabara katika kutekeleza moja ya nguzo za imani hasa kwa waumini wa dini ya Kiislamu na walipomaliza waliendelea na msiiamamo wao huku wakiimba: “Tunamtaka Kikwet, tunamtaka Kikwete…”
Kutokana na hali hiyo viongozi wa ngazi za juu wa Jeshi la Polisi walifika katika eneo hilo ili kujaribu kutuliza hali hiyobila mafanikio.
Kwanza alifika Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Kipolisi ya Kati (OCD), Wilbrod Mutafugwa akiongozana na baadhi ya askari lakini hakufanikiwa.
Mbali na askari wa kawaida walikuwa wametapakaa katika eneo hilo pia walifika askari waliokuwa na mabomu ya machozi na gari la maji ya kuwasha.
Kufika kwa gari hilo kuliamsha hisia kubwa za wastaafu hao ambao badala ya kukumbia walishangilia na kuwalazimisha askari hao kuwapiga mabomu na kuwamwagia maji hayo huku walikisogelea gari.
Baadhi yao walisikika wakisema kuwa hawaogopi huku wakidai kuwa Yesu Masihi na Mtume Muhamad nao walikufa hivyo hata wao kufa hawaoni tabu.
Hata hivyo vikosi hivyo havikuweza kuchukua hatua yoyote na badala yake waliendelea kuwaangali wazee hao waliokuwa wakidai haki yao huku wakiimbva kuwa wanamtaka Kikwete.
Baadaye alifika Msajili wa Mahakama ya Rufani, Francis Mtungi ambaye alifanya kikao cha dharua na uongozi wa mahakama hiyo kisha alitoka nje na kwenda kuzungumza nao hukua akiwa ameongozana na Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam ACP, Charles Kenyela.
Kabla ya kutoka nje Mtungi alisikika akiwaambia Polisi waondoe lile gari la Maji ya kuwasha akidai kuwa ni aibu kwani dunia yote inawaona.
Hata hivyo Mtungi licha ya kuwasihi waondoke na kuahidi kulifuatilia suala lao hilo na kuwahakikishia kulishughulikia Jumatatu, wastaafu hao hawakukubali badala yake waliendelea kukaa na kulala barabarani.
Hali hiyo ililazimisha Mahakama hivyo kuitisha tena kikao cha dharura saa tisa chini ya uongozi wa Jaji Kiongozi, Fakihi Jundu ambapo aliteuliwa pale pale jaji mwingine John Utwamwa kwa ajili ya kusikiliza na kutolea maamuzi kesi yao hiyo.
Sambamba na kumteua Jaji Utamwa pia mahakama hiyo ilipanga kesi yao hiyo iendeshwe kesho badala ya Jumatatu kama ilivyokuwa awali, lakini baada ya wakili wao Charles Semgalawa kuwapa taarifa hizo wastaafu hao walipinga wakitaka mambo yaishe jana hiyohiyo.
Ilibidi Kaimu Kamanda Kenyela aingilie kati na kuwasihi kwa upole ili waondoke lakini huku akiwataka warudi Ijumaa na kuwaahidi kuwa atakuwepo kuwapa ulinzi, walitaka kukataa hadi alipolazimika kuwapa muda wa dakika 15 kuondoka.
Wastaafu hao waliwanza kuondoka taratibu eneo hilo kuanzia saa 4:00 huku wakisisitiza leo kukutana na kuahidi kurudi kesho huku wakionya kutokudanganywa.
Akizungumzia suala hilo Msajili wa Kanda wa Mahakama Kuu Amir Msumi alisema kuwa jaji Mwaikugile ameamua kujiondoa katika kesi hiyo kwa mujibu wa taratibu na kanuni na kwamba hawaamini kuwa uamuzi huo ni chanzo cha hatua walizozichukua.
Alisema kisimsingi suala hilo lingekuwa limekwisha isipokuwa kwa kiasi kikubwa limecheleweshwa na wastaafu hao baada ya kuibuka makundi mawili ambayo yalikuwa yakivutana, moja lingine likitaka kukata rufaa na lingine likitaka kukazia hukumu ili walipwe.
Msumi aliongeza kuwa mahakama ilikuwa imeagiza mawakili wao wote wakutane waandaye maombi ya malipo ya pamoja ambayo yangesikilizwa Septemba 27, mwaka huu lakini siku hiyo jaji alikuwa likizo fupi.
"Kwa kuwa mimi sikuwa na mamlaka ya kisheria kulitolea maamuzi, hilo la kuongeza muda niliahirisha kesi hiyo na kuwapangia tarehe ya leo waje kutoa maombi hayo mbele ya Jaji," alisema Msumi.
Kesi hiyo kwa sasa iko katika hatua ya kukazia hukumu ya maridhiano ya Mahakama Kuu ya Septemba 12, 2005 iliyotolewa na Jaji Catherine Urio ambayo iliwapa ushindi wastaafu hao.
Katika kesi yao ya msingi namba 93 ya mwaka 2003 walikubaliana kuwa Serikali iwalipe kiasi chaSh.117bilioni, ambazo wanadai kuwa hadi sasa bado hawajalipwa.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)