Meneja
Chapa wa Tigo, Bw. William Mpinga (kulia) akimkabidhi ufunguo wa Bajaji mshindi
wa kwanza wa promosheni ya ‘Miliki Biashara Yako’, Bw.
Mohamed Ramadhani Mnjori (39) muuz nguo za mitumba, mkazi wa Ilala – Dar es
Salaam kwenye halfla ya makabidhiano iliyofanyika eneo la Soko Kuu la Kariakoo,
Dar es Salaam.
Meneja
Chapa wa Tigo, Bw. William Mpinga (kushoto) akimpa mkono wa pongezi mshindi wa
kwanza wa promosheni ya ‘Miliki Biashara Yako’ ibuka na Bajaji Bw. Mohamed
Ramadhani Mnjori (39) alipopanda kukagua Bajaji yake. Bajaji hiyo ina thamani
ya Tsh 6,700,000.
Meneja
Chapa wa Tigo, Bw. William Mpinga (kulia) akimkabidhi ufunguo wa Bajaji mshindi
wa pili wa promosheni ya ‘Miliki Biashara Yako’, Bw. Riziki
Lucas Kisemo (36) mfanyakazi wa viwandani, mkazi wa Makabe, Dar es Salaam. Tigo
tayari imelipia leseni ya barabani (Road license) na bima kwa ajili ya Bajaji
hizo. Anachotakiwa mteja sasa, ni kuanza biashara yake bila shida mara moja.
Meneja
Chapa wa Tigo, Bw. William Mpinga akimtambulisha mshindi wa tatu wa promosheni
ya ‘Miliki Biashara Yako’ Bw. Adam Saidi Kalulu (36) mkulima,
mkazi wa Kiluvya kabla ya kumkambidhi Bajaji yake mpya
mbele ya wanahabari na wananchi waliojitokeza eneo la Soko Kuu la Kariakoo
kushudia makabidhiano hayo.
Meneja
Chapa wa Tigo, Bw. William Mpinga (mwenye kofia ya Tigo) katika picha ya pamoja
na washindi watatu wa kwanza ya promosheni ya ‘Miliki Biashara Yako’ ibuka na
Bajaji wakati wa sherehe ya makabidhiano iliyofanyika leo eneo la Soko Kuu,
Kariakoo. Mteja wa Tigo anao
uwezo wa kujishindia Bajaji moja kila siku kwa muda wa siku 60 kwa kuongeza
vocha ya Tsh 1,000 tu kwa siku.
Mshindi
wa pili wa promosheni ya ‘Miliki Biashara Yako’, Bw. Riziki
Lucas Kisemo (36) mfanyakazi wa viwandani, mkazi wa Makabe, Dar es Salaam
akitoa ushuhuda mbele ya vyombo vya habari jinsi hapo zamani alipokuwa
akihangaika na kazi ‘ngumu ngumu’ ambazo zilikuwa hazimpi kipato cha kutosha cha
kuendeshea maisha yake. Mshindi huyo ametoa shukurani nyingi sana kwa Tigo na
ametoa rai kwa watanzania wengine waweze kushiriki. “Hakika Tigo imebadilisha
maisha yangu,” Riziki alisema. Pembeni yake ni Meneja Chapa wa Tigo, Bw. William Mpinga,
Bajaji
3 kati ya Bajaji 60 zilizoshindwa na washindi wa droo ya kwanza ya promosheni
ya ‘Miliki Biashara Yako’ zikipaki eneo la Soko Kuu, Kariakoo kabla ya
kukabidhiwa kwa washindi mapema leo. Zimebakia Bajaji 57 zakushindaniwa, droo
inayofuata itachezwa siku ya Jumatatu 29 Julai, 2013 kwa ajili ya kuwapata
washindi 7 wa wiki hii.
Wateja wanaweza kuendelea kushiriki kwa kuongeza salio mara nyingi wawezavyo
ili kujiongezea nafasi zaidi ya kujishindia Bajaji na kumiliki biashara zao
wenyewe.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)