Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Mzee Timoth Apiyo likiwazili Makaburini kwa kubebwa na Askari wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Jeneza likiingizwa kaburini.
Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda akiweka udongo kaburini.
Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda akiweka shada la maua kaburini.
Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda akijadiliana jambo na Mke wa hayati Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere wakati wa msiba huo.
WAZIRI
Mkuu Mizengo Pinda,ameongoza mamia ya waombolezaji kwenye mazishi ya
aliyekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Marehemu Timoth Apiyo,yaliyofanyika
nyumbani kwake kijiji cha Marasibora mkoani Mara.
Waziri
Pinda alitoa pole kwa familia na wakazi wa Kijiji cha Mara
Sibora,Wilaya ya Rorya na Mkoa wa Mara kwa kumpoteza kiongozi na
mzalendo aliyeitumikia nchi yake kwa uadilifu.
Wengine
waliohudhuria maziko hayo ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano
na Uratibu),William Lukuvi;Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue;
Makatibu Mkuu Viongozi wastaafu, Balozi Paul Rupia, Balozi Marten
Lumbanga na Philemon Luhanjo pamoja na mke wa hayati Baba wa Taifa, Mama
Maria Nyerere.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)