HAKUNA KANISA LILILOSHAMBULIWA KWA BOMU JIJINI DAR LEO - SULEMANI KOVA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

demo-image

HAKUNA KANISA LILILOSHAMBULIWA KWA BOMU JIJINI DAR LEO - SULEMANI KOVA

SelemanKovaKamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kova amesema Taarifa  zilizoenea kwamba Bomu limelipuka katika Kanisa la Kilutheri la Kiinjili Tanzania (KKKT), Kunduchi jijini Dar es Salaam zimeenea ndivyo sivyo na kwamba askari walikuwa wanapambana na majambazi.

Wakati taarifa zikiwa zimesambaa katika mitandao ya kijamii na mitaani kwamba  kuna kanisa la KKKT limeshambuliwa na bomu hivi punde, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kova amesema kwamba taarifa hizo sio za kweli na kwamba askari wa jeshi la polisi walikuwa wanapambana na majambazi karibu na eneo la kanisa hilo. 


Katika mapambano hayo polisi waliwarushia majambazi hayo bomu ili kuyakamata. "Wakati askari wetu wanapambana na majambazi hayo- waumini wa kanisa hilo  wamejitokeza kuwasaidia askari wetu. Naomba unisaidie kukanusha siyo kweli, nitazungumza na vyombo vingine vya habari kuweka sawa," amesema  Kamanda Kova hivi Punde.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Pages