Meneja wa Kinywaji cha Grandmalt Bi Consolata Adam
kulia akiwa na afisa mahusianao wa TBL Bi Doris malulu wakizungumza na
waandishi wa Habari jijini Dar Es Salaam juu ya uzinduzi wa tuzo za wanafunzi
wa vyuo vikuu nchini ambapo Tamasha la Kwanza litafanyika jumamosi hii
kwenye viwanja vya chuo kikuu Arthi na jumapili kwenye chuo kikuu cha Mkwawa
mkoani Iringa.
Dar es Salaam, April 16, 2012:
Kinywaji
maarufu cha Grand Malt leo kimezindua tuzo kwa wanafunzi wa elimu ya
juu zijulikanazo kama “Excel with Grand Malt”, huu ukiwa ni mwaka wa
tatu kwa tuzo hizi kutolewa.
Akizungumzia
tuzo hizo, meneja wa kinywaji cha Grand Malt Bi. Consolata Adam
alisema; Excel with Grand Malt ni tuzo za aina yake ambazo zimelenga
kutambua na kuthamini mchango wanaoonesha wanafunzi katika fani
mbalimbali nje ya masomo ya darasani. Tunatambua kuwa kazi kubwa ya
mwanafunzi anapokuwa chuoni ni kuhudhuria vipindi vya darasani na kupata
elimu, bali tunapenda pia kuwatambua wale wachache ambao wanakwenda
mbali zaidi na kufanya mambo ya maendeleo katika mazingira yao ya chuo.
Tuzo
hizi zilianzishwa mwaka juzi ambapo tuliweza kufika katika mikoa sita
na kufikia vyuo vipatavyo ishirini. Kwa mwaka huu mchakato utaanza mwezi
Aprili hadi June, na Mikoa itakayohusika ni pamoja na Dar es salaam,
Morogoro, Iringa, Dodoma, Kilimanjaro na Mwanza ambapo vyuo vipatavyo 20
vitashiriki. Kama ilivyokuwa miaka iliyopita, fani zitakazoshindanishwa
ni Ubunifu (Innovation), Michezo (sports), Utamaduni na burudani
(Culture & Entertainment) na Mazingira na Huduma za jamii
(Environment & social responsibilities). Kama ilivyo ada, washindi
katika fani hizi watajipatia zawadi mbalimbali toka Grand Malt ikiwa ni
pamoja na pesa za kununulia vitabu na vyeti vya ushindi.
Kwa
sasa natangaza rasmi kuwa tunzo hizi zimezinduliwa rasmi na mkoa wa
kwanza utakuwa ni hapa Dar Es Salaa ambapo tunatarajia kufanya tamasha
kubwa kwenye viwanja vya chuo kikuu cha Chuo kikuu Artdhi siku ya
jumamosi kisha jumapili tutafanya tamasha la ufunguzi kwenye Viwanja vya
chuo cha Mkwawa mkoani Iringa na kutakuwa na burudani na zawadi nyingi
na zaidi kutakuwa na GrandMalt baridi na hakutakuwa na kiingilio
chochote. Alisema Bi. Consolata.
Akielezea
umuhimu wa Tuzo hizo, meneja masoko wa TBL Bw. Fimbo Butallah alisema;
Alisema tunafurahi sana kuona vyuo vyote vilipokea tuzo hizi kwa furaha
kubwa, hii ni kwa sababu wanatambua umuhimu wake.
Kupitia tuzo hizi
ambazo zitakuwa zikitolewa kila mwaka, Grand Malt inatoa changamoto kwa
vijana walio vyuoni kuona umuhimu wa kujituma na kufanya mambo mengi na
makubwa zaidi ya kufaulu mitihani ya darasani tu.
Tunaomba viongozi wa
serikali za wanafunzi na viongozi wa vyuo kuendelea kutoa ushirikiano
kama walivyofanya mwaka jana ili kuleta ufanisi zaidi katika tuzo za
mwaka huu. Kama ilivyo kawaida, utaratibu utakuwa ule ule ambapo wanchuo
watapendekeza majina ya vijana wanaoamini kuwa wamefanya mambo makubwa
ndani ya vyuo vyao katika tasnia zilizotajwa hapo
awali, kisha kufuatiwa na kipindi cha kupiga kura ambapo washindi
watapatikana. Alimaliza Bw. Butallah.
Kwa
upande wake Afisa uhusiano wa Tbl bi Doris Malulu Alisema GrandMalt kwa
kuzingatia umuhimu wa juhudi za serikali katika kuhamasisha jamii
kutunza mazingira kwa kupanda miti mwaka huu Grand Malt itafanya zoezi
maalum kwenye kila chuo kwa kupanda miti imara itakayosaidia kutunza na
kuboresha mazingira ya vyuo hivyo ili kuandaa mazingira bora ya kusomea
ya wanafunzi wa sasa na wa vizazi vijavyo ambapo mkoani Iringa zoezi
hilo litafanyika jumatatu April 22,2013 katika vyuo vya Mkwawa,Ruaha na
Tumain na Mkoani Dodoma zoezi hilo litafanyika kwenye vyuo vya UDOM na
St Johns siku ya
jumatatu April 29,2013 asubuhi , kisho zoezi hilo litaendelea katika
mikoa ya Morogoro,kilimanjaro,Mwanza na Dar Es Salaam.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)