MAAFISA HABARI WA SERIKALI WATEMBELEA BUNGE NA KUSHIRIKI ZOEZI LA UPANDAJI WA MITI CHUO KIKUU CHA DODOMA(UDOM) - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

MAAFISA HABARI WA SERIKALI WATEMBELEA BUNGE NA KUSHIRIKI ZOEZI LA UPANDAJI WA MITI CHUO KIKUU CHA DODOMA(UDOM)


Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Habari Bw. Raphael Hokororo akiwafundisha maafisa habari na mawasiliano wa serikali kutoka Wizara, Taasisi, wakala, mashirika ya Umma, mikoa na wilaya upigaji wa picha bora za mnato kwa matumizi ya habari wakati wa kuhitimisha kikao cha maafisa hao mjini Dodoma.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw. Clement Mshana ambaye alikua miongoni mwa waalikwa waliohudhuria kikao kazi cha maafisa habari na mawasiliano wa serikali akiongea na mafiasa hao mjini Dodoma.
Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali wakiwa ndani ya Ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma kufuatia mwaliko wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara.
Maafisa habari na mawasiliano wa serikali wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutoka nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
Baadhi ya viongozi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Mkurugenzi wa Idara hiyo Bw. Assah Mwambene (wa nne kutoka kushoto) na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Usajili wa Magazeti Bw. Raphael Hokororo (wa pili kutoka kushoto) wakiwa wamesimama ndani ya ukumbi wa Bunge kuwasalimia waheshimiwa wabunge mara baada ya kuombwa na Mh. Spika wakiwaongoza maafisa habari wa serikali.
Maafisa Habari na Mawasiliano wa serikali wakiwasili Chuo Kikuu cha Dodoma kushiriki zoezi la upandaji wa miti chuoni hapo ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika kuhifadhi mazingira ya chuo hicho.
Mhasibu mkuu msaidizi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Swalehe Chondoma akishiriki zoezi la upandaji wa miti katika kampasi ya chuo kikuu cha Dodoma.
Naibu katibu mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akizindua zoezi la upandaji wa miti lililowahusisha mafisa habari wa Serikali katika kampasi ya chuo kikuu Dodoma.
Maafisa habari na Mawasiliano wa Serikali wakiendelea na zoezi hilo Chuo kikuu cha Dodoma.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages