Tamasha la Kuchangia Mtoto wa Kike Nchini Uingereza - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tamasha la Kuchangia Mtoto wa Kike Nchini Uingereza

Mstahiki Meya akifungua Tamasha.
Mama Balozi akiwaonyesha wageni Rasmi Mameya vitu mbalimbali  vitakavyouzwa kwa ajili ya kuchangia mfuko huu.
Mtahiki Meya akiangalia sehemu ya chakula ya Tanzania.
kutoka Kushoto Mh balozi wa Grenada Ruth Elizabeth Rouse, Mtahiki Meya Christopher Buckmaster na Mama Balozi Joyce Kallaghe.
Mama Kiondo akiwa kikazi zaidi kuitangaza Tanzania Pics .
Mama Balozi Akipakwa Hina kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa elimu
Mama Balozi akimkabidhi Mayorese Mrs. Anne Hobson baada ya kununua kitenge katika banda la Tanzania .
Mayorese Mrs. Anne Hobson katika banda la Tanzania.
wateja wakinunua bidhaa kutoka banda la Tanzania.
Sherehe ikiendeleaPics By Frank Eyembe.
Ukumbi wa Royal Borough of Kensington.Pics By Frank Eyembe.
---
Salaam,

Jumuiya ya Commonwealth Countries League (CCL) inayoshirikisha nchi hamsini na nne (54) duniani kutoka katika jumuiya ya madola iliandaa tamasha maalum siku ya jumamosi tarehe 3.11.12 kwa ajili ya kuchangia mfuko wa kumsaidia na kumwezesha msichana kusoma elimu ya sekondari.

Historia ya Commonwealth Countries League ilianzishwa rasmi kutoka kwa  baadhi ya wanawake mnamo mwaka 1923 nchini Australia kwa ajili ya kusaidia kutangaza uelewa wa haki sawa kati ya wanawake na wanaume waliopo nchi  mbalimbali zilizo ndani katika jamuiya  ya madola.

Tamasha hili  lilifanyika Royal Borough of Kensington chini ya uongozi kutoka kwa Mh. Balozi wa Grenada Ruth Elizabeth Rouse ambaye ndio raisi wa jumuiya hiyo akisaidia na makamu wake mama Balozi Joyce Kallaghe. Wageni Rasmi walikua  Wastahiki Mameya wa Worshipful  Royal Borough of Kensington na Chelsea - Councillor Christopher Buckmaster na  Mrs. Anne Hobson Shughuli ya mwaka huu iliandaliwa na wake za mabalozi kutoka katika jumuiya za Madola hamsini na nne (54) ili kuchangisha pesa kwa njia ya kuuza vitu mbalimbali vya asili kama chakula, urembo, maua, vinywaji n.k. Fedha zote zilizopatikana zilipelekwa kusaidia mfuko huu wa Elimu kwa ajili ya kumsomesha mtoto wa kike.

Aidha Mama Balozi Joyce Kallaghe aliongeza kwa kusema ''Elimu ni Ufunguo Wa Maisha kumsomesha mwanamke ni kuiwezesha jamii nzima hivyo vipaumbele vyote vimeelekezwa kwa kwa ajili ya kuwasomesha watoto wa kike walio maskini au wanaoishi katika mazingira magumu ambao wana uwezo wa kuendelea kusoma elimu ya sekondari katika nchi za jumuiya ya Madola". Tangu  mwaka 2011/2012 mfuko wa Elimu wa CCL ushawawezesha watoto wa kike 364 kutoka nchi 25  ikiwapo Tanzania. Pia aliwasihi wadau kuwa wazalendo kwa kuchangia mfuko huu kwa kuwasiliana kupitia barua pepe ccl.edfund@googlemail.com 

Kiasi cha paundi mia moja hamsini (£150) na Mia nne na hamsini (£450) zinatosha kumsomesha msichana kwa mwaka mzima

Asanteni

Urban Pulse Creative

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages