Wanafunzi Buguruni Viziwi na Balozi wa Airtel AY-waomba Watanzania kuchangia vifaa vya kufundishia. - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wanafunzi Buguruni Viziwi na Balozi wa Airtel AY-waomba Watanzania kuchangia vifaa vya kufundishia.

 
Balozi wa Airtel  nchini Ambwene Yessaya (AY) (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa chekechea ya shule ya msingi Buguruni Viziwi walipotembelea shule hiyo mwishoni mwa wiki hii.Airtel kwa kushirikiana na BAMVITA wanaendesha mradi maalum utakaowezesha wanafunzi hao wenye uhitaji maalum kupata vifaa vya kujifunzia.
Meneja huduma za jamii wa Airtel Hawa Bayumi akiangalia ujuzi wa wanafunzi wa shule ya Buguruni viziwa alipotembelea shule hiyo mwishoni mwa wiki hii. wakati AIRTEL na Balozi wao msanii AY walipofanya ziara maalum ya kuhamasisha jamii kuchangia wanafunzi hao wa shule ya msingi Buguruni viziwi kupata vifaa vya kujifunzia kwa kushirikiana na BAMVITA.
Mwalimu wa shule ya msingi Buguruni Viziwi akiwapa ujumbe wanafunzi wa shule hiyo baada ya kutembelewa na wafanyakazi wa Airtel, kutoka kushoto ni mwamlimu mkuu wa shule hiyo bi Winfrid Jeromia, akifuatiwa na Meneja huduma za jamii wa Airtel Hawa Bayumi na Airtel Ambassador Ambwene Yessaya (AY). Airtel kwa kushirikiana na BAMVITA wanaendesha mradi maalum utakaowezesha wanafunzi hao wenye uhitaji maalum kupata vifaa vya kujifunzia
Meneja huduma za jamii wa Airtel Hawa Bayumi akiongea na wanafunzi wa shule ya Buguruni Viziwi mwishoni mwa wiki hii wakati ambapo airtel walitembelea shule ya msingi viziwi kuhamasisha upatikanaji wa vifaa vya kufundishia pamoja na nyenzo mbalimbali kupitia mradi maalumu wa kuchangia vitabu unaoendeshwa na Airtel kwa kushirikiana na BAMVITA, kushoto ni Mwalimu wa shule hiyo bi Judith Kaneno akifuatiwa na Airtel Ambassador ajulikanae kwa jina la AY( Ambwene Yessaya) kulia ni Mwalimu mkuu bi. Winfrid Jeromia.


==========  =========  ==========

Wanafunzi Buguruni Viziwi na Balozi wa Airtel AY-waomba Watanzania kuchangia vifaa vya kufundishia.

Ni moja kati ya shule zitakazofaidika na mradi wa Airtel na BAMVITA

Wanafunzi wa shule ya Buruguni viziwi  wameomba watanzania na wadau mbalimbali kuchangia ili kufanikisha upatikanaji wa vifaa vya kufundishia pamoja na nyenzo mbalimbali kupitia mradi maalumu wa kuchangia vitabu unaoendeshwa na Airtel kwa kushirikiana na BAMVITA. Wanafunzi hao waliosema hayo wakati Airtel pamoja na balozi wake AY walipotembelea shuleni hapo mwisho mwa wiki hii.

Wanafunzi wa shule ya buruguni viziwi ambao mbali na masomo ya darasani pia wanafundishwa kazi za stadi, walionekana kufanya kazi za stadi za mikono ikiwemo kutengeneza shanga pamoja na mazulia madogo ya miguu, wametia hamasa na kuthibithisha kwamba  wakiwezeshwa na kupatiwa nyenzo wanauwezo mkubwa sana wa kufanya shughuli za stadi na ubunifu.

Akiongea katika ziara hiyo Meneja huduma za jamii wa Airtel Hawa Bayumi alisema “leo tumetembelea shuleni hapa ikiwa ni mwendelezo wa utaratibu wetu katika kubainisha mahitaji ya ziada ambazo shule hizi zenye mahitaji maalumu zinahitaji. Shule ya Buruguni viziwi ni moja kati ya shule zitakazofaidika Mradi huu unaoshirikisha Airtel na BAMVITA una lengo la kusaidia kuendeleza kiwango cha Elimu hapa nchini na kutoa nafasi kwa jamii yetu kuweza kushiriki na kuchangi elimu ya msingi kwa watoto wenye mahitaji maalum. ‘

Naye Balozi wa Airtel AY Ambwene Yesaya alisema “ Tunawashukuru watanzania kwa kuitikia wito na kuanza kuchanga na tunaendelea kutoa wito kwa watanzania kuendelea kuchangia kwa kutuma neno “Vitabu” kwenda namba 15626 na kwakufanya hivyo kila SMS utakayotuma utakuwa umechangia shilingi 200 au kuchangi kiwango chochote kupitia Airtel money 0788 041361 ambapo jina la fumbo ni VITABU.

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Buguruni Viziwi bi. Winfrid Jeromia alikuwa na haya ya kusema”tunaishukuru sana Airtel kwa kuweza kuja na mradi kama huu wa kuweza kuinua Elimu hapa nchini na kurahisha mazingira yetu ya ufundishaji hapa shuleni. Tunawaomba watanzania wengine na makampuni mengine makubwa yajitokeze kwa wingi kuweza kuchangia katika mradi huu ili kuinua wigo wa Elimu hapa nchini.

Kampeni hii ya kuchangia vifaa kwa shule zenye mahitaji maalumu inayoendeshwa na Airtel kwa kushirikiana ilizinduliwa Agosti 23 2012 na itaendelea kwa muda kwa mienzi mitatu. Kwa kuanzia shule tatu za jijini Dar es Salaam ambazo ni Uhuru Mchanganyiko, Sinza Maalum, na Buguruni Viziwi zitafaidiaka na mradi huu.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages