Makamu wa Rais Dkt . Bilal kufungua Mkutano wa saba wa Kimataifa wa Wafanyabaishara wanawake jijini Dar es salaam kesho - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Makamu wa Rais Dkt . Bilal kufungua Mkutano wa saba wa Kimataifa wa Wafanyabaishara wanawake jijini Dar es salaam kesho

Mwenyekiti wa Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) Fatma Riyami (kulia) akiongea na waandishi  wa habari (leo) jijini Dar es salam juu ya Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Wanawake wafanyabiashara wa Nchi ya Mashariki mwa Afrika unaofanyika Tanzania kwa mara ya kwanza na unaotarajiwa kufunguliwa na Makamu wa Rais wa Tanzania Dr. Mohamed Gharib Bilal  . Kushoto ni Makamu wa Mwenyekiti wa TWCC Anna Matinde. Mkutano huo unafunguliwa tarehe 22.10.2012 katika Hotel Kunduchi Beach.
…………………………………………………………….
Na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es salaam

Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilal anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Wanawake wafanyabiashara wa Nchi ya Mashariki mwa Afrika unaonza kesho  jijini Dar es salaam kwa lengo la kuimarisha mtandao wao.

 Kauli hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) Fatma Riyami wakati  akiongea na waandishi  wa habari  Ofisi kwake.
Amesema kuwa Mkutano huo ambao ni wa saba(7) unafanyika nchini Tanzania kwa mara ya kwanza tangu walipoanzisha ushirikiano huo wa wanawake wafanyabiashara kwa nchi za  Afrika Mashariki.

Mwenyekiti huyo amesema kuwa wajumbe wa Mkutano huo wanatarajiwa kutoka katika Nchi za Kenya, Uganda, Rwanda , Burundi, Ethiopia , Sudan Kusini na mwenyeji Tanzania.

Amesema kuwa  Mkutano huo utakuwa fursa nzuri kwa wajumbe kutoka nchi zote saba kubadilishana uzoefu katika kazi ya kuwainua kiuchumi wakimama na kuimarisha Mtandao wa Wafanyabiashara wanawake katika Nchi za Afrika Mashariki.

 Ameongeza kuwa hatua hiyo itasaidia kufanya soko la wafanyabiasha wanawake wa Afrika Mashariki kuwa kubwa na hivyo kuwainua kiuchumi wakimama.

 Aidha Bibi Fatma Riyami amesema kuwa TWCC imeanzisha matawi katika Mikoa ya Kagera, Mwanza, Pwani, Dodoma, Mbeya, Dar es salaam na Arusha ikiwa na lengo la kutaka kuwa karibu na wafanfanyabiashara wanawake kwa nia kuimarisha Umoja wao.

 Wakati huo Mwenyekiti huyo amewasisitiza wajumbe wa Mkutano huo kufika katika Hoteli hiyo ifikapo saa 1.30 Asubuhi , Mgeni rasmi atafungua mkutano huo saa 2.00 kamili

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages