Mwananchiwa Kijiji cha Kilombero Nd. Bakari Mtumwa Silima akiwasilisha
kilio cha Wananchi waKijiji hicho cha ufinyu wa Huduma yaMaji safi
mbele ya Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi hapo Skuli
yaKilombero Wilaya ya Kaskazini B.
NduguBakari Omar wa Shehia ya Kilombero akielezea kadhia inayowapata
Watoto waokatika kivuko kinachojaa maji msimu wa masika wakati
wanapokwenda kwenye masomoyao.
Mbunge wa Jimbo la Kitope BaloziSeif
Ali Iddi akijibu na kufafanua
baadhi ya kero zinazowakabili wananchi waShehia ya Kilombero katika
harakati zao za kila siku za maisha.Kulia ya Balozi ni Mkuu wa Wilaya ya
Kaskazini B Nd. Khamis Jabir Makame na Kushoto yake ni Mkewe Mama
AshaSuleiman Iddi
Mbunge waJimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi akipeana mikono na
Wananchi wa Shehia ya Kilombero mara baada ya kupokea kerona matatizo
yanayowakabili Wananchi hao
--
Wananchi wa shehia ya Kilombero iliyoko Wilaya ya Kaskazini B wameuomba
Uongozi wa Jimbo lao, Wilaya na Serikali Kuu kuangalia uwezekano wa
kuwapatia huduma ya Umeme itakayosaidia kutanzua tatizo la maji
linalowakabili kwa muda mrefu sasa.
Ombi hilowamelitoa mbele ya Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali
Iddi aliyefika Kijijini hapo kusikiliza matatizo na kero zinazowakabili
wananchi hao hapo katika viwanja vya skuli ya Kilombero.
Ndugu Bakari Mtmwa Silima akiwasilisha Kero za Wananchi hao alimueleza
Balozi Seif kwamba licha ya juhudi zinazochukuliwa naViongozi wa Jimbo
hilo lakini bado huduma ya Maji safi inaendelea kuwa mtihani kwao.
Nd. Bakari alisema harakati za uchimbwaji wa Kisima cha maji safi kwa
ajili ya Wananchi wa Shehia hiyo unaendelea vyema lakini tatizo
linalojitokeza ni upatikanaji wa huduma za umeme kufikia eneo hilo.
“ Utaratibu wa kupelekea umeme Kilombero juu kilipo kisima hicho
unafikia masafa ya Kilomita moja. Lakini mbali ya huduma hiyo ya maji
pia sisi wananchi tunahitaji huduma hiyo kwa matumizi ya kawaida”.
Alisisitiza Ndugu Bakari Mtumwa.
Naye Ndugu Bakari Omar alielezea kilio kinachowapata watoto wa eneo hilo
cha ukosefu wa kivuko wakati wanapokwenda skuli hasa wakati wa msimu wa
mvua kubwa.
Alisema kivuko kinacholigawa eneo la kitongoji chao naskuli ya Kilombero
huzidiwa na maji wakati wa masika na kutishia maisha ya wanafunzi hao
wakati wanapotaka kuvuka.
Akijibu hoja za Wananchi hao wa Shehia ya Kilombero , Mbunge wa Jimbo la
Kitope Balozi Seif Ali Iddi aliwataka Wananchi hao kuendelea kuwa na
ustahamilivu na juhudi zitaendelea kufanywa ili kuona huduma ya maji
safi inapatikana kwa uhakika katika eneo hilo.
Alisema Uongozi wa Jimbo, Wilaya na Hata Serikali Kuu unaelewa tatizo la
usumbufu wa huduma ya maji safi unaowapata Wananchi wa Kilombero.
“ Ukweli usiofichika kwamba maji ni uhai wa kilakiumbe. Kwa kulifahamu
hili mimi binafsi ninaposikia kiliocha maji katikamaeneo maeneo yoyote
Nchini huamua kulivalia njuga hadi lifikie ufanisi”.Alisisitiza Balozi
Seif.
Balozi Seif aliwahakikishia Wananchi hao kwamba yeyena viongozi wenzake
wa Jimbo watafanya jitihada za kuwasiliana na Taasisi mbalimbali ili
kuona namna gani wanaweza kusaidiana kulitatua tatizo la Umeme ambalokwa
sasa linahitaji uwezo wa ziada.
“ Licha ya uchimbwaji wa Kisima hicho cha maji kuondoatatizo la Wananchi
hao lakini bado kazi iliyopo hivi sasa ya huduma ya umemeinahitaji
gharama kubwa”. Alisisitiza Balozi Seif.
Alisema upo uzoefu unaoonyesha kwamba tatizo laukosefu wa maji safi
katika maeneo mengi linaonekana kusababishwa na nguvu ndogo zinazotokana
na mashine zinazowekwa kwenye visima vya maji.
Akizungumzia kivuko kiliopo kati ya Kilombero Skuli na Kilombero Juu
Balozi Seif aliagiza kupatiwa makisio ya gharama za kazi ya Matengenezo
ya eneo hilo muda wowote kuanzia sasa ili kukamilisha kazi hiyo na kutoa
faraja kwa watoto na wakaazi wa eneo hilo.
Balozi Seif alisema hatua ya kuondosha usumbufu huoinawezekana
kukamilishwa ndani ya wiki moja baada ya kupatikana kwa Kifusi na
Makalvati.
Mapema Mke wa Mbunge wa Jimbo Hilo la Kitope Mama Ash aSuleiman Iddi
aliwakumbusha Wananchi hao kuendelea kuthamini juhudi zinazochukuliwa na
Viongozi wao katika kuwatatulia kero zinazowakabili.
Uchimbaji wa kisima cha Maji safina salama kwa ajili ya Shehia hiyo ya
kilombero unaendelea katika eneo la Kilombero juu ukigharamiwa na Mbunge
wa Jimbo hilo.
Na
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)