Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad
akibadilishana mawazo na Rais wa Zanzibar Dkt Ali MohdShein, kwenye
viwanja vya hoteli ya Bwawani walipokutana kwa ajili ya Baraza
laEid-El-Fitri,jana tarehe 19/08/2012.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazala Mapinduzi Dkt Ali Mohd Shein,
akiwa pamoja na viongozi wakuu wa Zanzibar naviongozi wengine kwenye
viwanja vya hoteli ya Bwawani wakati wa sherehe zaBaraza la Eid-El-
Fitri.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa ZanzibarMaalim Seif Sharif Hamad (kulia) na
Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume, kila mmoja akiwa na
shauku ya kutaka kumweleza mwenzake chochote,walipokutana katika hoteli
ya Bwawani kwa ajili ya Baraza la Eid-El-Fitri.Viongozi hawa ndio
walioasisi maridhiano ya kisiasa Zanzibar na kupatikana Serikali ya Umoja
wa Kitaifa.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa ZanzibarMaalim Seif Sharif Hamad
akisalimiana na viongozi mbali mbali katika viwanjavya hoteli ya Bwawani
walipokutana kwa ajili ya Baraza la Eid-El-Fitri,jana tarehe
19/08/2012.Picha na Salmin Said-Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais
Zanzibar
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)