Baadhi
ya Maiti zilizookolewa kutoka katika Meli ya Skagit iliozama hapo jana
zikitambuliwa na Ndugu zao na kuruhusiwa Kuzichukuwa kwa ajili ya
Kufanya taratibu za mazishi hapo katika Viwanja vya Maisara Mjini
Zanzibar.
Balozi
wa Marekani Nchini Tanzania Learnhat Alfonso wakatikati akionekana na
huzuni Baada ya kuziona Maiti zilizookolewa katika Meli iliozama hapo
jana katika Bahari ya Chumbe Zanzibar.Balozi alifika katika Viwanja vya
Maisara ili kuona namna shughuli za kushughulikia maiti zinavyoendelea.
Mama
alietambulika kwa Jina la Bitatu Uyelo ambae amenusurika na Kupoteza
Mtoto wake wa miezi tisa katika Ajali ya Meli ya Skagit iliozama hapo
jana katika Bahari ya Chumbe ikitokea Dare es salaam.
Waziri
wa Mamboya ndani wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Emanuel Nchimbi
alifikakatika Eneo lililohifadhiwa Maiti wa Ajali ya Meli ya Skagit ili
kutambuliwa na Ndugu zao na Kupata maelezo kwa Daktari Kiongozi hayupo
pichani Hapo katika Viwanja Vya Maisara Zanzibar.Picha Kwa Hisani Ya Michuzi Blog
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)