MASHUJAA KUENZIWA KITAIFA TAREHE 25 JULY 2012 KATIKA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA JIJINI DAR ES SALAAM - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

MASHUJAA KUENZIWA KITAIFA TAREHE 25 JULY 2012 KATIKA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA JIJINI DAR ES SALAAM

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki (katikati) akiongea na waandishi wa habari Katika viwanja vya Mnazi mmoja leo jijini Dar es Salaam kueleza namna mkoa ulivyojipanga kufanikisha sherehe za  maadhimisho ya siku ya mashujaa itakayofanyika kitaifa tarehe 25, Julai 2012 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam
Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakitoa heshima kwenye mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa katika viwanja vya mnazi mmoja leo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya sherehe za maadhimisho ya kumbukumbu ya mashujaa.
Askari Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) watakaoshiriki kwenye gwaride wakati wa maadhimisho ya siku ya mashujaa wakiendelea na mazoezi katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
Kiongozi wa mabalozi wa nchi za Afrika wanaoishi nchini Tanzania  Balozi Ibrahim Mukubi kutoka  Uganda akiweka shada la maua kwenye mnara wa kumbukumbu ya mashujaa leo jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya sherehe ya siku ya mashujaa itakayofanyika tarehe 25, Julai 2012.

Na. Aron Msigwa – MAELEZO.    Dar es salaam.
 
Wananchi wa mkoa wa Dar es salaam wameombwa kujitokeza kwa wingi wakati wa sherehe za maadhimisho ya kumbukumbu ya  Siku ya Mashujaa itakayofanyika kitaifa katika viwanja vya Mnazi mmoja tarehe 25 Julai 2012  jijini Dar es salaam.
 
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam , Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki amesema maandalizi ya maadhimisho hayo yamekamilika na kufafanua kuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete.
 
Amesema katika maadhimisho hayo kwa upande wa mkoa wa Dar es  salaam  baadhi ya barabara  zitafungwa ikiwemo barabara ya Nyerere, Uhuru na Bibi Titi Mohamed ili kuhakikisha usalama kwa wale wote watakaohudhuria maadhimisho hayo na kuongeza kuwa katika kuboresha maadhimisho hayo kamati ya maadhimisho itaweka luninga katika maeneo yote muhimu ili kuwawezesha wananchi kuona yanayotendeka wakati wa maadhimisho hayo.
 
Aidha Bw. Meck Sadiki amesema kuwa maadhimisho hayo ni kumbukumbu muhimu katika historia ya Tanzania kwa kuwaenzi mashujaa waliojitoa muhanga katika jitihada za kuikomboa na kuilinda Tanzania.
 
“ Maadhimisho haya ni kumbukumbu muhimu sana katika historia ya nchi yetu kwani tunawaenzi mashujaa wetu waliojitoa muhanga katika jitihada za kuikomboa, kuilinda na kudumisha amani na utulivu wan chi yetu”

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages