Taifa Stars imetolewa kwenye mechi za mchujo za Kombe la Mataifa ya
Afrika baada ya kufungwa kwa penalti na wenyeji Msumbiji (The Mambas)
katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa ulioko Zimpeto pembeni kidogo
ya Jiji la Maputo.
Refa Bennett Daniel alipopuliza filimbi ya kumaliza dakika 90 za
pambano hilo timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1, hivyo kwa mujibu wa
kanuni za mashindano hayo yanayoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa
Miguu Afrika (CAF) mikwaju ya penalti ikatumika kupata mshindi.
Katika mechi ya kwanza iliyochezwa Dar es Salaam, Februari 29 mwaka huu timu hizo
zilitoka sare ya bao 1-1.
Msumbiji ndiyo walioanza kupata bao dakika ya 9 lililofungwa na
mshambuliaji Jeremias Sitoe akiungnisha krosi ya Elias Pelembe ambaye
mabeki wa Taifa Stars walifikiri ameotea.
Stars ilisawazisha bao hilo dakika ya 89 likifungwa kwa kichwa na
Aggrey Morris kutokana na mpira wa kona uliopigwa Amir Maftah.
Mikwaju ya penalti tano tano walioifungia Stars walikuwa Amir
Maftah, Shabani Nditi na Shomari Kapombe wakati Aggrey Morris na Kevin
Yondani.
Kwa vile The Mambas nao walikosa mbili ikabidi iongezwe penalti
moja moja. Waliofunga kwa upande wa Stars walikuwa John Bocco, Frank
Domayo na Mrisho Ngassa wakati Mbwana Samata alikosa.
Akizungumzia pambano hilo, Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen aliwapongeza wachezaji wake kwa kupambana hadi dakika ya mwisho.
"Tulikuja Maputo tukijua kuwa tunatakiwa kufunga bao, tumeweza
kufunga bao ingawa katika dakika za mwisho. Unajua linapokuwa suala la
penalti chochote kinaweza kutokea, na ndivyo ilivyokuwa," alisema Kim.
Taifa Stars itarejea nyumbani Juni 19 mwaka huu, ambapo itaaondoka
hapa saa 4.40 asubuhi kwa kupitia Nairobi, Kenya na kutua Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 1.50 usiku.
Kikosi kilipngwa hivi; Juma Kaseja, Shomari Kapombe, Erasto
Nyoni/John Bocco, Aggrey Morris, Kevin Yondani, Shaabani Nditi, Mrisho
Ngasa, Frank Domayo, Thomas Ulimwengu/Haruna Moshi, Mbwana Samata na
Mwinyi Kazimoto/Amir Maftah.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)