ais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Bw. Deo Mwanyika, Makamu wa
Rais wa Kampuni ya Barrick Tanzania baada ya kuibuka mchangiaji mkubwa
kwa kutoa dola za Kimarekani laki 5 kwa ajili ya kuchangia taasisi ya
Mkapa Hiv/Aids Foundation Jumanne Juni 5, 2012 usiku katika hoteli ya
Kilimanjaro jijini Dar es salaam. Kushoto ni Rais Mstaafu wa Awamu ya
Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi na kulia ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu
Mzee Benjamin William Mkapa aliyeandaa hafla hiyo iliyoweza kukusanya
shilingi bilioni 3.2 na kuvuka malengo ya harambee hiyo kwa asilimia
sita
Rais Jakaya Kikwete, akimkabidhi picha ya kuchora Ofisa Mtendaji
Mkuu wa Kampuni ya UNDI Consulting Group Limited, Bw Philip Makoka
aliyoinunua kwa shilingi milioni 20 wakati wa Harambee ya kuchangia
fedha programu ya Mkapa Fellows inayoendeshwa naTaasisi ya Mkapa
HIV/AIDS iliyofanyika Dar es Salaam kwenye hoteli ya Kilimanjaro Hyatt
Regency jijini Dar es salaam. Kulia ni mchoraji wa picha hiyo, Bwana
Muzu
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na Rais Mstaafu wa Awamu
ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi (kushoto) na Rais Mstaafu wa Awamu ya
Tatu Mzee Benjamin William Mkapa baada ya kuwa mgeni rasmi katika
harambee ya kuchangia Taasisi ya Mkapa HIV/AIDS foundation na kusaidia
kukusanya shilingi bilioni 3.2 nauvuka malengo ya harambee hiyo kwa
asilimia sita.PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)