Kaka
mkubwa wa marehemu aliyekuwa Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Willy
Edward Ogunde, George Ongiri Ogunde (wa kwanza kulia) akishirikiana na
ndugu, jamaa na waandishi wa habari, kubeba mwili wa mhariri huyo,
aliyefariki dunia ghafla jana usiku eneo la Forest Hill, mjini
Morogoro. Mwili huo ulikuwa unatolewa chumba cha kuhifadhia maiti
Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kusafirishwa kwenda
jijini Dar es Salaam kwa maandalizi ya mazishi katika Kijiji cha
Mugumu kilichopo wilaya ya Serengeti, mkoani, Mara..
Mbunge
wa Jimbo la Morogoro, Azizi Abood, akiwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa
Kampuni ya New Habari (2006), Husein Bashe wakisubiri kuuona mwili wa
Willy Edward
Baadhi
ya waandishi wa habari akiwemo Mbunge wa Morogoro mjini, Azizi Abood,
wakiwa na huzuni walipokuwa wakisubiri kutoa heshima za mwisho katika
Hospitali ya Rufaa ya Morogoro, muda mfupi kabla ya mwili kusafirishwa
Dar es Salaam.
Mkuu
wa mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (kulia) akisikiliza jambo kutoka kwa
kaka mkubwa wa marehemu aliyekuwa mhariri mkuu wa gazeti la Jambo Leo,
Willy Edward Ogunde, George Ongiri Ogunde muda mfupi kabla ya kuanza
safari ya kwenda jijini Dar es Salaam kwa maandalizi ya mazishi katika
kijiji cha Mgumo kilichopo wilaya ya Serengeti mkoani Musoma. wa
pili kutoka kulia ni Katibu Tawala wilaya ya Morogoro, Alfred Shao na
kaka mkubwa upande wa baba, Isack Ugunde.Picha Kwa Hisani Ya Father Kidevu Blog
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)