Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts Limited, inayochapisha
gazeti la Jambo Leo na jarida la Jambo Brand Tanzania, Juma Pinto
(kushoto) na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Benny Kisaka (wa pili kushoto)
wakiwa kwenye msiba wa aliyekuwa Mhariri Mkuu wa Jambo Leo, marehemu
Willy Edward Ogunde ulioopo nyumbani kwa kaka wa marehemu Mburahati, Dar
es Salaam leo asubuhi. Wiily amefariki ghafla leo alfajiri mjini
Morogoro alikokuwa akihudhuria semina ya siku moja ya masuala ya Sensa.
Kutoka kulia ni ndugu zake marehemu; Dennis Ongiri, Joseph Rabach na
Julius Rabach.
Waandishi
wa habari wa gazeti la Jambo Leo na Jarida la Jambo Brand Tanzania
wakishiriki kwenye msiba wa aliyekuwa Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo
Leo, marehemu Willy Edward. Mwili wa marehemu Willy unasafirishwa mchana
huu kutoka Morogoro kwenda kuhifadhiwa Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili, Dar es Salaam. Taratibu za mazishi zinaendelea kuratibiwa
kwa ushirikiano wa ndungu na viongozi wa Jambo Concepts, lakini kwa
mujibu wa Kaka wa marehemu Rabach ni maazishi yatafanyika nyumbani kwao
marehemu, mjini Mugumu Wilaya ya Serengeti, mkoani Mara. Siku ya
mazishi itatangazwa baadaye.
Waombolezaji wakimfariji mjane wa marehemu Willy Edward, Rehema
Akina mama waombolezaji wakiwa kwenye msiba
Mpiga picha wa TBC, Mary Hondo, akimfariji Rehema.
Mtoto wa mwisho wa marehemu, Willy Edward, Caren akiwa katika msiba
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)