Ile dhana ya kwamba shule zote za kata ziko
katika
mazingira magumu na hazifanyi vema katika maendeleo ya elimu siyo
inaanza kupingwa kwa vitendo,utafiti uliofanywa na mwandishi kutoka
HakiElimu mkoani Arusha umegundua kuwa ingawa shule nyingi za kata
hazifanyi vyema na kukabiliwa na changamoto lukuki, kuna baadhi ya shule
za sekondari za Kata
ambazo zina maendeleo mazuri kitaaluma kushinda hata zile shule
Kongwe za Serikali na Shule nyingi za binafsi.
Mfano wa shule za kata zinazofanya vema ni shule ya sekondari ya kata ya
Kaloleni iliyoko wilayani Arusha. Shule hii ilianzishwa mwaka 1998 ni
moja ya shule zinazofanya vema kielimu ambapo katika mtihani wa kitaifa
wa mwaka jana wa kidato cha nne , shule hii ilishika nafasi ya 12 kati
ya shule 137 za mkoa wa Arusha zilizofanya mtihani huo na kushika nafasi
ya 179 kati ya shule 3108 zilizofanya mtihani huo nchini .Shule hii
ilikuwa na jumla ya watahiniwa 179 waliofanya mtihani huo ambapo
watahiniwa 15 walipata daraja la kwanza, 17 wakapata daraja la pili, 47
walipata daraja la tatu, 85 wakapata daraja la nne na 15 walifeli kwa
kupata daraja 0.
|
Vibao mbali mbali kuonesha sehemu na huduma mbalimbali shuleni hapo |
|
|
|
|
|
Baadhi ya magari ya walimu na wageni yakiwa yameegeshwa shuleni hapo kusubiri wamiliki wao wakiwa kazini
Mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya sekondari Kaloleni, Mrs Machange M.J
Tofauti na shule nyingine za kata , shule hii ina maabara kwa
ajili ya masomo ya sayansi ambapo mwandishi alifanikiwa kutembelea
maabara za somo la Fizikia, Kemia na Bailojia. Pia jambo lingine la
utofauti ni mazingira ya shule kuwa mazuri ikiwemo sehemu ya kuegeshea
magari ya wafanyakazi na wageni ambapo mwandishi aliduwazwa na neema
aliyoiona ya eneo hilo tofauti ya shule nyingine za kata zenye mazingira
magumu. Hii huenda ikawa ni kutoka na mazingira ya shule hii kuwa
katikati ya jiji la Arusha eneo la Kaloleni. |
|
Maabara
kwa shule ya sekondari ya Kaloleni si jambo geni kwani zipo maabara za
kila somo la sayansi.hii ni maabara maalumu ya elimu ya viumbe
(Baiolojia) |
|
Maabara ya Chemistry |
|
Maabara ya Physics |
Pamoja na mafanikio hayo, shule hiyo inakabiliwa na changamoto
mbalimbali ikiwemo mlundikano wa wanafunzi ambapo kwa sasa ina jumla ya
wanafunzi 967 wa kidato cha kwanza mpaka cha nne, huku kukiwa na idadi
ndogo ya walimu na kulazimika kuajiri walimu waliohitimu kidato cha sita
kuokoa jahazi. Pia shule hiyo ni moja ya shule zilizopokea wanafunzi
wasiojua kusoma na kuandika katika kidato cha kwanza ambapo jumla ya
wanafunzi watatu walikuwa na maksi mbaya sana katika mtihani uliotolewa
kwa kupata maksi chini ya tano katika mitihani iliyofanywa ya kuhesabu
kusoma na kuandika kufuatia wimbi kubwa la wanafunzi wasiojua kusoma na
kuandika nchini kuchaguliwa kujiunga na masomo ya Sekondari jambo ambalo
lilipigiwa kelele na wadau mbalimbali likiwemo shirika la HakiElimu. Habari na picha zote na Abraham Lazaro alieyekuwa Arusha
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)