Timu
ya Taifa ya Gambia (The Scorpions) imewasili nchini jana (Juni 7 mwaka
huu) saa 5.30 usiku kwa ndege ya Kenya Airways tayari kwa ajili ya mechi
dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
Msafara wa timu hiyo wenye watu 31 wakiwemo wachezaji 22 unaongozwa na
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Vijana na Michezo wan chi hiyo, Malang Jassey.
Viongozi
wengine ni Ofisa Utawala wa timu Modou Sowe, Kocha Luciano Machini,
makocha wasaidizi Peter Bonu Johnson na Lamin Sambou, Kocha wa makipa
Alhagie Marong, mtaalamu wa tiba mbadala (physiotherapist) Pa Matarr
Ndow, Mtunza vifaa Sanna Bojang na Daktari wa timu Kalifa Manneh.
Wachezaji ni Musa
Camara, Abdou Jammeh, Momodou Futty Danso, Lamin Basmen Samateh, Ousman
Koli, Pa Saikou Kujabi, Mustapha Kebba Jarju, Yankuba Mal Ceesay, Demba
Savage, Saihou Gassama, Alieu Darboe, Momodou Ceesay, Pa Modou Jagne,
Tijan Jaiteh, Bubacarr Sanyang, Christopher Allen, Musa Yaffa, Sulayman
Marr, Mamut Saine, Hamsa Barry, Ali Sowe, Omar Colley na Saloum Faal.
Gambia
‘The Scorpions’ itafanya mazoezi yake ya kwanza leo (Juni 8 mwaka huu)
saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume wakati kesho muda huo
huo itafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa.
Kambi
ya Taifa Stars iko vizuri ambapo leo jioni timu itafanya mazoezi Uwanja
wa Taifa. Pia kesho itafanya mazoezi kwenye uwanja huo huo kuanzia saa
11 jioni baada ya Gambia kuwa wamemaliza.
Jumamosi
saa 4 kamili asubuhi kutakuwa na mkutano kati ya makocha wa timu zote
mbili; Mdenmark Kim Poulsen wa Taifa Stars na Mtaliano Luciano Machini
wa The Scorpions wakiwa na manahodha wao na Waandishi wa Habari
utakaofanyika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)