Madam Ritah Paulsen akipokea mtoto kutoka kwa mshiriki huyu aliyekuja nae katika shindano hilo kabla kuanza kuimba. |
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Zantel ambao ni wadhamini wakuu wa EBSS 2012 Awaichi Mawalla akichangia damu |
Na Mwandishi Wetu Dodoma
PAZIA la shindano la Epiq Bongo Star
Search (EBSS) kwa mkoa wa Dodoma limefungwa rasmi huku vipaji kibao
vikiwa vimejitokeza na kuwavutia majaji.
Kilichovutia
zaidi ni washiriki wa miaka 16 ambao walionekana kuimba vema na kuwa
kivutio hata kwa washiriki wenzao waliofurika katika ukumbi wa Royal Village.
Akizungumzia shindano hilo Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya Benchmark Production inayoandaa shindano hilo
Ritha Paulsen alisema kuwa amevutiwa na wingi wa washiriki mkoani hapa
hasa idadi ya washiriki wasichana pia.
Alisema kuwa ikiwa ni mara ya kwanza
kuruhusu washiriki wa miaka 16 kuingia katika usaili wa EBSS 2012
ameshuhudia hazina kubwa ya vipaji vya washiriki wa umri huo.
Katika
usaili huo kulikuwa na washiriki wa aina mbalimbali wakiwamo wanafunzi,
wafanyabiashara ndogondogo, vijana wa mitaani na wadau wengineo wa
muziki.
Kwa
kuthamini umuhimu wa akina mama na watoto mshiriki aliefika kuonesha
kipaji chake katika ukumbi huo alipewa nafasi ya kuimba ili aweze kuwahi
kuondoka.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Zantel ambao ni wadhamini wakuu wa EBSS 2012 Awaichi Mawalla
mbali na kuvutiwa na ushiriki wa vijana waliojitokeza pia alihamasisha
upimaji wa damu kwa kuchangia damu kwa kituo cha damu mkoani Dodoma.
“
Kwa kupitia EBSS 2012 tunataka kuwafikia vijana sio tu katika muziki
bali pia hata katika kuhamasisha masuala mbalimbali yahusuyo jamii kama
vile hili la kuchangia damu na mengineo” alisema Awaichi.
Washindi watakaopatikana watatangazwa
baadae katika vyombo vya habari. Baada ya Dodoma kwa sasa inafuata
Zanzibar ijumaa ijayo katika eneo la Ngome Kongwe
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)